Na Mwandishi Wetu
BONDIA Omari Kimweri kupanda tena
ulingoni April 15 nchini Australia katika ukumbi wa Melbourne Pavilion
kwa ajili ya kugombania mkanda wa Dunia baada ya kumchapa
Michael Camelion wa Philippines kwa point
Bondia huyo Mtanzania mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia
amewashukuru watanzania kwa duwa zao walizo mwombea adi kufanikiwa kupata ushindi uliomwezesha kupata nafasi yakugombania mkanda wa Dunia
Kimweri mpaka sasa ameshacheza mpambano 18 akipoteza michezo 3
katika rekodi za ubora yeye ni namba 1 nchini
Australia na ni namba 98 katika rekodi za Dunia
bondia huyo anaetamba katika anga zakimataifa kupitia mchezo wa masumbwi Duniani amendelea kuomba watanzania kuwa waendelee kumuombea duwa na ato waangusha kamwe
kwa kuwa yeye ni mtanzania na kitovu chake kimezikia Tanzania kwa hiyo anajivunia utanzania wake akiwa ugaibuni
Kimweri alitoa shukrani za
kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka
sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni
Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli ,
Rajabu Mhamila 'Super D'
Kocha wa Tanzania Prison Remmy
Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa
pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge
Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga
No comments:
Post a Comment