Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
HEKAHEKA zimeanza Visiwani Zanzibar ambapo wagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Wawakilishi wameanza kupigana vikumbo kuwania nafasi hiyo huku sura mpya za vijana wenye damu mbichi zikijitokeza kuchuana na mkongwe aliyechukua tena fomu ya kutetea nafasi yake Mhe Pandu Ameri Kificho.
Kificho
ni Spika wa Bunge la Wawakilishi kwa muda wamiaka 25 sasa ambapo
wanachama wa CCM Zanzibar tayari wameanza kutilia mashaka uamuazi wa
spika huyo aliyechukua fomu za kugombea tena akitaka kuendelea na
kuongoza kiti cha uspika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, jambo,
inalozua maswali mengi yasiyo na majibu.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar,
walitoa maoni yao juu ya sakata hilo na kusema kuwa Kificho hakustaili
kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kijacho bali alitakiwa kuiga mfano wa
baadhi ya viogozi kama Spika Pius Msekwa na wengine walioamua kuachia
ngazi kwa kujiuzuru madaraka na kuwaachia vijana wenye hali ya kuongoza
ili kupata radha mpya katika Bunge hilo la Wawakilishi.
Naye
mgombea, Mahamud Muhamed Mussa, alisema kuwa amejitokeza kuchukua fomu
ili kuwania nafasi hiyo kutokana na uwezo alionao na Zaidi akijiandaa
kuongoza kisasa Zaidi na kuleta mabadiliko ili Bunge la Wawakilishi liwe
lakisasa na kuendana na kaulimbiu ya Mhe Rais wa Jamhuri ya 'Hapa kazi
tu', alisemaMussa.
''Kiukweli
Kificho sasa anaelekea kuwaudhi Vijana ambao nao sasa ni muda wao wa
kuongoza ili waweze kuchangia mengi waliyonayo ili kuendana na Kasi ya
Rais wa awamu ya tano Mhe Dkt. Magufuli, Kificho amekalia kiti cha Spika
Bunge la Wawakilishi kwa muda wa miaka 25 sasa ni kwa nini asipumzike
na kuwaachia vijana wafanye kazi, sidhani kama bado ana jipya'', alisema
Mwanachama mmoja wa CCM aliyejitambulisha kwa jina la Kijeshi.
Aidha
Wanachama hao walikwenda mbali Zaidi kwa kukumbushia wakati wa zoezi la
Kura ya maoni kuhusu Serikali mbili,ambapo Mhe. Kificho alionekana
kwenda kinyume na msimamo wa Chama chake wa Serikali mbili huku yeye
akionyesha msimamo wake Zaidi wa kudai Serikali tatu akidai 'eti' ni
msimamo wa Baraza la Wawakilishi.
Waliojitokeza
kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Pandu Ameri Kificho,
Mahamud Muhamed Mussa, Zuberi Ali Maulid, Muhamde Ali Amhed, Jajh
Janeth, Sadifa Juma, David Mwakanjuki, Perera Silmg na Abdallah Wazisi,
ambapo mchuano mkali unaonekana kuwa kwa ni kati ya Spika aliyemaliza
muda wake akijaribu kutetea kiti chake, Pandu Ameri Kificho, Mahamud
Muhamed Mussa na Jaji Janeth Sekihola.
No comments:
Post a Comment