Saturday, April 16, 2016

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ASHINDA KWA POINT AKIWA NCHINI PANAMA


BONDIA IBRAHIMU CLASS AKIWA NA MIKANDA YAKE YA UBINGWA WA AFRIKA  WPBF JUU NA CHINI NI U.B.O AFRIKA
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na bondia Shane Mosley ambaye alishawai kucheza na Floyd Mayweather na kuonesha upinnzani mkubwa kushoto ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa hapa ni baada ya kushinda mpambano wake na Zapir Rasulov wa Russia kwa point
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na mpinzani wake Zapir Rasulov wa Russia baada ya kumshinda kwa point 

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Mtanzania Bingwa wa Afrika wa mikanda ya WPBF na U.B.O Afrika Ibrahimu Class 'King Class Mawe' april 15 mwezi uhuu amefanya maajabu baada ya kumtwanga bila huruma

Bondia 

Zapir Rasulov wa Russia na kufanikiwa kumpiga kwa point katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya

Convenciones Vasco nchini

Panama City, Panama 

 Class anakuwa bondia wa kwanza kumpiga bondia huyo katika mapambano yake 30 aliyocheza ambapo kati ya hayo mapambano 27 ameshinda kwa K.O na matatu kashinda kwa point 

 bondia huyo arikuwa na rekodi ya kutopigwa ata mpambano mmoja ambao aliocheza katika michezo yake yote

Class ameweka dowa katika michezo yake na kuwa bondia wa kwanza kutoka afrika kumpiga bondia huyo anaesifika uku ugaibuni

 Bodia King Class Mawe baada ya kuibuka na ushindi uho amesema ushindi ni wa watanzania wote kwani yeye amekuwa mtumishi wao tangia mpambano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa ubingwa alipokwenda nchini Zambia na ufanikiwa kumdunda bondia Mwansa Kabinga  katika mpambano uliofanyika Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia hii ilikuwa june 8 ,2014  na kushinda kwa TKO ya raundi ya tisa na kufanikiwa kurudi na mkanda wa WPBF Afrika

hivyo natarajia kuendeleza kuitumikia Tanzania na watu wake kupitia mchezo wa masumbwi nchini

bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha likiongozwa na kocha mkongwe kabisa Habibu Kinyogoli akisaidiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye amekuwa akimshauli katika mapambano yake mblimbali nchini

bondia huyo anataraji kurudi nchini wakati wowote kwa ajili ya maandalizi ya mpambano mwingine wa asumbwi utakaomkabili hivi katibuni

No comments:

Post a Comment