BONDIA IBRAHIMU CLASS AKIWA NA MIKANDA YAKE YA UBINGWA WA AFRIKA WPBF JUU NA CHINI NI U.B.O AFRIKA |
Bondia Ibrahimu Class 'King Class
Mawe' kulia akiwa na bondia Shane Mosley ambaye alishawai kucheza na
Floyd Mayweather na kuonesha upinnzani mkubwa kushoto ni Rais wa ngumi
za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa hapa ni baada ya kushinda mpambano
wake na Zapir Rasulov wa Russia kwa point
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na mpinzani wake Zapir Rasulov wa Russia baada ya kumshinda kwa point Na Mwandishi Wetu BONDIA Mtanzania Bingwa wa Afrika wa mikanda ya WPBF na U.B.O Afrika Ibrahimu Class 'King Class Mawe' april 15 mwezi uhuu amefanya maajabu baada ya kumtwanga bila huruma Bondia Zapir Rasulov wa Russia na kufanikiwa kumpiga kwa point katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Hotel yaConvenciones Vasco nchiniPanama City, PanamaClass anakuwa bondia wa kwanza kumpiga bondia huyo katika mapambano yake 30 aliyocheza ambapo kati ya hayo mapambano 27 ameshinda kwa K.O na matatu kashinda kwa pointbondia huyo arikuwa na rekodi ya kutopigwa ata mpambano mmoja ambao aliocheza katika michezo yake yoteClass ameweka dowa katika michezo yake na kuwa bondia wa kwanza kutoka afrika kumpiga bondia huyo anaesifika uku ugaibuniBodia King Class Mawe baada ya kuibuka na ushindi uho amesema ushindi ni wa watanzania wote kwani yeye amekuwa mtumishi wao tangia mpambano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa ubingwa alipokwenda nchini Zambia na ufanikiwa kumdunda bondia Mwansa Kabinga katika mpambano uliofanyika Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia hii ilikuwa june 8 ,2014 na kushinda kwa TKO ya raundi ya tisa na kufanikiwa kurudi na mkanda wa WPBF Afrikahivyo natarajia kuendeleza kuitumikia Tanzania na watu wake kupitia mchezo wa masumbwi nchinibondia huyo anaenolewa na jopo la makocha likiongozwa na kocha mkongwe kabisa Habibu Kinyogoli akisaidiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye amekuwa akimshauli katika mapambano yake mblimbali nchinibondia huyo anataraji kurudi nchini wakati wowote kwa ajili ya maandalizi ya mpambano mwingine wa asumbwi utakaomkabili hivi katibuni |
No comments:
Post a Comment