Kijana
mjasiriamali Theresia Maliatabu (Kulia) akimkabidhi picha aliyoichora
kwa ubunifu wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso (Kushoto) kama
shukrani yake kwa Airtel baada ya kuwezeshwa kupitia mpango wa Airtel
FURSA "Tunakuwezesha" kwa kupatiwa vifaa vya kuboresha biashara yake.
Katikati ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya mkutano wa mwezi wa wafanyakazi
Airtel uliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao makuu Morocco jijini
Dar es salaam.
XXXXXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Kupitia
mradi wa Airtel fursa ambao umekuwa ukitoa misaada mbalimbali kwa vijana
nchini kwa kuwawezesha kufanikisha ndoto zao, ambapo mmoja kati ya
kijana anaejihusisha na ubunifu wa sanaa za uchoraji aliyenufaika na
mradi huo, Bi, Theresia Maliatabu leo Juni 01. 2016, amemtembelea
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bw. Sunil Colaso na kumzawadia picha yake
aliyoichora mara tu Airtel Fursa kumpatia Kijana huyo vifaa vya
kidigital katika semina iliyofanyika miezi miwili iliyopita na
kuchagua vijana wawili walioweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi
katika semina hiyo kwaajili ya kuboresha ubunifu wao.
Akikabidhi
zawadi hiyo Theresia alisema” vifaa hivyo vinanisaidia kubuni baadhi ya
michoro ambayo ni ya kisasa zaidi, lakini hasa inanisaidia mazoezi
katika kuchora na vile vile inanisaida kama sehemu ya kutangaza biashara
yangu kupitia social media”.
“Napenda
kuwaambia vijana wenzangu kwamba wajiamini na vipaji walivyokuwa nazo
wasikate tamaa kwani kila kitu kinawezekana na wasiache kuchangamkia
fursa kama hizi zinapojitokeza, aliongeza Theresia
Mpaka
sasa Airtel imefanya semina nyingi sana za mafunzo ya biashara ya
ujasiriamli hapa nchini katika mikoa mbali mbali na kuweza kufikia
vijana wapatao 4000. Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA
utaendelea kutoa warsha hizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili
kuhakikisha inafikia vijana wengi zaidi.
Vijana
wanahamasishwa wanaposikia nafasi kama hii popote walipo , kuchangamkia
kwa kuhudhuria kwani elimu inayotolewa ni bure kabisa bila gharama
yoyote.
No comments:
Post a Comment