Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo
Chambo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar
es Salaam leo mchana wakati akimkaribisha Ofisa Masoko Mwandamizi wa
Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), kuzungumza na wanahabari
kuhusu mbio hizo zitakazofanyika kesho kutwa. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), akizungumzia kuhusu mbio hizo.
Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday (kulia), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo.
Mwanafunzi Rachel
Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Mwenzake Ali
Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wa mbio
hizo.
Wanahabbari wakichukua taarifa hiyo.
Waratibu wa mbio hizo
wakionesha fulana zitakazotumiwa na watoto watakao kimbia mbio hizo.
Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha
Tanzania (RT), Peter Mwita, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday,
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.
Dotto Mwaibale
NAIBU
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mbio za Watoto za Azania Kids Run
2016,
zitakazofanyika Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016,
zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa
Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi katika kinyang'anyiro hicho
kitakachokuwa na mbio za kategori tano.
Gidabuday
amebainisha kuwa, maandailizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda
vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto
wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha
wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.
"Mbio
hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia
kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,
zikihusisha watoto chini ya miaka 16, ambako Naibu Waziri Wambura
atakuwa mgeni rasmi," alisema Gidabuday.
Amewasisitiza
wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu
bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza
la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho
la Riadha Tanzania (RT).
Gidabuday
ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto
watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati
wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa
kukimbia.
"Barabara
zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum
ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa
watakaohitaji kupatiwa huduma hizo," amesema Gidabuday katika mkutano na
wanahabari Dar es Salaam.
Ofisa
Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za
washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka
wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la
kihistoria.
"Mshindi
wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh.
150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye
vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10
watapata kifuta jasho cha sh. 15,000," amesema.
Katika
mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa
mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000
na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne
hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.
Aidha,
amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh.
75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh.
40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama
kilivyotajwa hapo juu.
Pia
kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini
ya miaka mitatu, ambako washindi washindi wote watafunguliwa akaunti
katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na
begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.
No comments:
Post a Comment