FRED SAYUNI |
Na Mwandishi Wetu
Haidari Mchanjo |
Katika ali iliyo ya kawaida kwa mashabiki wa michezo baada ya kucheza mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama Ndondo Cup sasa timu za Goms United na Keko Furniture kukutana katika masumbwi ambapo Goms united inawakilishwa na bondia Haidari Mchanjo na KekoFurniture anatoka Fred Sayuni
Mabondia hawo wamesaini mkataba na watazipiga siku ya Septemba 15 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Indoor Stadium akizungumza baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Sayuni amesema kama kawaida yake anawambia mashabiki wake wote wa Keko kuwa yupo vizuri na anajiandaa kushinda ushindi wa kishindo
ambapo kwa sasa anafanya mazoezi ya kutosha ili awafurahishe mashabiki wake ili waweze kumpa sapoti ya mana awze kuendelea na kipaji chake mbele zaidi
Nae Mchanjo amejinasibu kwa kusema Sayuni ni bondia wa zamani hivyo nitamfanyia kitu mbaya kama nilivyo mfanyia Cosmas Cheka mana nilimpiga kama begi nae afanye mazoezi ili nisije nikamuaibisha mbele ya mashabiki wake
nawaomba mashabiki wangu wote wale wa goms pamoja na viunga vyake waje kuangalia kazi nitakayofanya siku hiyo
Akizungumzia mpambano mratibu wa mapambano ya ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi wakati Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atazipiga na Geoger Dimoso na Vicent Mbilinyi atavaana na Saidi Mpoma 'Kidedea' wakati Mohamedi Kashinde atakumbana na Sadiki Momba na Imani Daudi ataoneshana umwamba na Paul Kamata
Na mpambano mwingine utawakutanisha Faraji Sayuni na Issa Nampepeche Ramadhani Shauri atakumbana na Said Amani wakati Mwinyi Mzengela atakumbana na Kassimu Rajabu 'Boxer Mnyama' Saidi Zungu na Tonny Rashidi
mapambano hayo yameandaliwa na kampuni ya ngumi za kulipwa ya Super D Boxing Promotion inayoendelea kuinuwa vipaji vya mabondia mbalimbali nchini ili kujikuzia kipato na kujiweka nafasi nzuri kwa mabondiakucheza kula wakati
No comments:
Post a Comment