Friday, August 17, 2018

MABONDIA IBRAHIMU CLASS NA BAINA MAZOLA KUZIPIGA KESHO P.T.A SABASABA


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza kupima kwa ajili ya kupigana kesho Agost 18 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba kuzipiga na Baina Mazola 'Simba' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Baina Mazola akizungumza na vyomba vya habari baada ya kupima uzito kwa ajili ya kuzipiga kesho jumamoso agost 18 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza kupima kwa ajili ya kupigana kesho Agost 18 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba kuzipiga na Baina Mazola 'Simba' Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Baina Mazola 'Simba' leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Agost 18 kesho jumamosi katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano uho wa raundi 8

akizungumza mara baada ya kupima uzito Class amesema yeye ni kiboko ya watoto wadogo ivyo ameamua kucheza na mazola ili amuoneshi kitu gani anafanya kwa kuwa ajacheza mda mrefu sana nchini Tanzania ivyo kuwaomba wapenzi wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi ili kuja kushudia kazi yake nzuri waliyoikosa kwa mda mrefu nawa akikishia nitampiga raundi za awali kwani kwangu anma ujanja alisema class

Nae Baina akijibu mapigo hayo amesema hizo ni mbwembwe mwisho wa siku yeye ndio anakuwa mshindi kwa kuwa yeye ni simba sitokubali kupigwa kirahisi kwani class ana maajabu ndio kwanza anakutana na kazi ngumu kutoka kwangu kwingine kote alikuwa anacheza na mabondia wachovyu nawaomba mashabiki mjitokeze kwa wingi ili mshudie ninavyo mchakaza class bila ya huruma alisema Mazola 

Mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine yatakayo wakutanisha Mada Maugo na Charles Misanjo kutoka Malawi 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini

No comments:

Post a Comment