Friday, May 21, 2010

HATMA YA GAllAS KWENDA A.KUSINI BADO


Hatma ya Gallas kwenda A.Kusini kitendawili

PARIS, Ufaransa
KOCHA wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Raymond Domenech amesema kuwa, hataki kumpeleka mchezaji William Gallas katika mechi za fainali za Kombe la Dunia endapo beki huyo wa Arsenal, hatakuwa katika hali nzuri hadi mwishoni mwa mwezi Mei.
Awali, kocha Domenech alisema kuwa, Gallas atakuwa ni mmoja wa wachezaji 24 atakaowaita katika kikosi chake, lakini juzi akakiambia kituo cha televisheni ya Ufaransa channel TF1 kuwa, beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 32, anaweza kuwa amepona majeraha yake yanayomkabili kabla ya Mei 27 Ufaransa kufunga safari kwenda Tunisia kwa ajili ya kuweka kambi ya mazoezi.
Gallas aliwasili katika kambi ya timu hiyo Jumamosi ili kupigania kujiweka fiti kwa ajili ya fainali hizo.
Hata hivyo, Domenech alisema kuwa, Gallas hatakwenda Tunisia endapo hatakuwa tayari kucheza.

No comments:

Post a Comment