Friday, May 21, 2010

tTWIGA YAITAJI SAPOTI YA WATANZANIA

Twiga Stars yazidi kujiamini

Na Addolph Bruno

WAKATI timu ya taifa ya Wanawake ya Eritrea ikitarajia kuwasili nchini leo kwa ajili ya mechi ya kuwania kufuzu michuanio ya Afrika, wenyeji timu ya taifa ya wanawake 'Twiga Stars', wametamba kuwazibua katika mechi hiyo.
Awali, Twiga Stars iliiondosha Ethiopia katika kwa jumla ya mabao 4-2, hivyo ikishinda mechi ya Jumapili, itakuwa imejiweka katika mazingira mazuri ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, nahodha wa timu hiyo, Sofia Mwasiliki, alisema wanaamini mchezo huo utakuwa rahisi kutokana na maandalizi waliyofanya.
Alisema makocha wao, Boniface Mkwasa na Adolph Rishard waliwaandaa vizuri kabla ya kuondoka kwenda kuongeza ujuzi wa kufundisha mpira nchini Brazili.
"Mechi hii ni yan kawaida kwetu, hatuwezi kubabaika nayo, tutashinda tu,"alisema Sofia.
Alisema wenzake wamejipanga kuhakikisha wanapeperusha bendera ya Taifa katika michuano hiyo kwa kuwachapa wapinzani wao na kutinga fainali za michuano hiyo.
Eritrea wanatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ndege ya shirika la ndege la Misri wakiwa na wachezaji 23.

No comments:

Post a Comment