Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 6, 2010

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TANGA ASIMAMISHWA UONGOZI


Kajembe apigwa chini uongozi TRFA

Na Oscar Assenga,Tanga

KATIBU mkuu wa chama cha soka mkoani Tanga,TRFA Salim Kajembe amesimamishwa uongozi katika chama cha soka mkoani hapa (TRFA) na kutakiwa kutojihusisha na shughuli za ukatibu wa chama hicho kuazia sasa.

Kwa mujibu wa barua iliyolifikia gazeti hili,ni kuwa maamuzi ya kumsimamisha Katibu huyo yalifikiwa katika mkutano wa kamati ya utendaji ya TRFA baada ya kuketi mapema hivi karibuni mkoani hapa.

Katika kikao ambacho kimefanyika mkoani hapa chini ya makamu mwenyekiti TRFA Mohamed Mhina Seleboss kilieza kuwa kimemsimamisha katibu huyo kwa mujibu wa ibara ya 13 ya katiba yake kifungu cha pili .

Barua hiyo iliyosainiwa na Seleboss imemtaka Kajembe kukabidhi vitu na mali ya chama hicho mara moja kwa katibu msaidizi wa chama hicho Fransis Kabelwa baada ya kuipata barua hiyo.

Hata hivyo barua hiyo haikueleza kwa undani wa sababu za kumng"oa madarakani Katibu huyo wala tuhuma zinazo mkabili zaidi ya kusisitiza kuwa hatma ya maamuzi hayo inategemea mkutano mkuu wa mwisho wa TRFA.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...