Marquee
tangazo
Sunday, June 6, 2010
POLISI MBEYA YAUA MAJAMBAZI MATATUKWA KUYAMIMINIA RISASI
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Marekani Irak, Jenerali Odierno
POLISI MBEYA YAUA MAJAMBAZI MATATUKWA KUYAMIMINIA RISASI
moses johnngwat
-POLISI MBEYA YAUA MAJAMBAZI MATATUKWA KUYAMIMINIA RISASI
-NI BAADA YA KUINGIA KWENYE MTEGO WA POLISI
-YADAIWA YALIKUWA YAKIVIZIA KUWAPORA WAFANYABIASHA WA MBAO WALIOKUWA NA SHEHENA YA FEDHA
Na Moses Ng’wat,
Mbeya.
JESHI la polisi wilayani Rungwe mkoani Mbeya,limefanikiwa kuwauwa majambazi watatu kati ya watano kwa kuwapiga risasi baada ya mapambano makali ya kurushiana risasi.
Majambazi hao waliuawa wakiwa katika harakati za kuwateka wafanyabiashara wa mbao wa mji wa Tukuyu, ambao wanadaiwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha, wakiwa njiani kwenda kununua mzigo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani hapa, Advocate Nyombi alisema tukio hilo lilitokea juni 3 majira ya saa 3:00 za usiku katika kijiji cha Nditu wilayani Rungwe.
Alisema baada ya jeshi hilo kupewa taarifa na raia wema kuwa kuna kundi la watu waliodhaniwa kuwa na nia ya kufanya uhalifu katika eneo la tukio,jeshi hilo liliamua kuweka mtego kwa kufanya doria ambapo baada ya muda mfupi walifanikiwa kuona kundi la watu watano wakiwa wamevalia makoti mazito.
Nyombi alisema baada ya askari kulifikia kundi hilo la watu liliwata wajitambulishe, lakini nao kwa upande wao walitoa amri ya namna hiyo kwa askari, hali iliyosababisha kutoelewana na ndipo mmoja kati yao alianza kufyatua risasi hovyo, jambo lililoyowalazimu polisi kujibu mapigo.
Alisema katika purukushani hizo majambazi watatu waliuawa kwa kupigwa risasi, huku wawili wakifanikiwa kukimbia,lakini hata hivyo siku ya pili ya tukio polisi walifanikiwa kumkamata mmoja kati ya majambazi hao waliofanikiwa kukimbia akiwa kwa mganga wa kienyeji akitibiwa majeraha ya risasi.
Hata hivyo kamanda Nyombi hakuwa tayari kutaja jina la jamazi hilo lililokuwa likitibiwa kwa mganga wa jadi kwa madai kuwa kungevuruga utaratibu wa kumpata jambazi mwingine ambaye hajakamatwa,lakini pia hakuweka wazi kama mganga huyo kakamatwa.
Kamanda Nyombi, alisema kati ya majambazi hayo waliouawa ni mmoja tu alitambuliwa kwa jina la Barik Martin (24),mkazi wa kijiji cha Lufilyo wilayani Rungwe,ambaye taarifa zake zinaonyesha kuwa alitoka jela Aprili 26 mwaka huu alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka mitatu.
Aidha, kamanda Nyombi alisema baada ya kupekua miili ya majambazi hao askari walifanikiwa kukuta bunduki moja aina ya ‘Short gun Pump Action’, maganda mawili ya risasi,na risasi nane zilizokuwa katika mfuko wa koti la mmoja wa majambazi hao, ambapo wengine walikutwa na panga mbili.
Kwa mujibu wa kamanda Nyombi uchunguzi zaidi unaendelea juu ya tukio hilo ili kumpata mmoja wa majambazi hao ambaye hajapatikana bado na pia kubaini iwapo majambazi hao wana mtandao mkubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment