Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 5, 2010

MISS DAR CITY CENTER 2010 KUPATIKANA LEO JIJINI


Kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Dar City Centre 2010, kinatarajia kufanyika Juni 5 kwenye Hotel ya Moven pick jijini Dar es Salaam, huku mrembo wa kwanza wa shindano hilo akinyakua kiasi cha shilingi Milioni moja(1000000) na wapili laki saba(700000) na wa tatu akinyakua kiasi cha laki tano(500000)

Mbali na zawadi hizo kwa washindi hao, pia zawadi kwa washindi waliobaki wataondoka na kifuta jasho cha shilingi 100000(laki moja moja0.

Katika shindano hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Millennium promoters, kundi la Machozi Band, sambamba na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ pamoja na Chege anayetamba na nwimbo wa ‘Mkono mmoja weka juu” watapagawisha mashabiki watajkaojitokeza kuangalia warembo hao.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Fortunatus Faustine, alisema kuwa katika shindano hilo ambalo linatarajia kuanza majira ya saa mbili usiku,kiingili kitakuwa ni kiasi cha shilingi 25,000, kwa muda wa kawaida na getini itakuwa ni shilingi 30,000.mbali na hilo pia kwa upande wa VIP ambapo itakuwa pamoja na chakula cha usiku, ni shilingi 50,000.

Kwa Upande wake mratibu wa kituo hicho cha Dar City Centre, Catheline John, alisema kuwa tiketi za shindano hilo zimeanza kuuzwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Best Bite-Namanga, Savannah Lounge, Movenpick- Gift Shop, Chiken Hut-MIlimani City, Rose Garden -Pub, Best Bite -Namanga.

Pia Catheline alisema kuwa warembo hao ambao mpaka sasa wanajifua katika hotel ya Lamada chini ya aliyekuwa miss Tabata pia alishiriki shindano la Miss Tanzania, Flora Florence(22).

Aliwataja baadhi ya warembo hao kuwa ni pamoja na Glory Mosha (20), Agness Francice (20), Bahati Chande (20), Kiren Mohammed (20), Sara Nasoro (20), Suraina Merwiro (23), Neema Jackob (2o), Neema Alen (18), Mariam Hassan (19), Sara Said (20), Nance Mane (20) na Anabela Isaya(21).
miss Dar city center kupatikana leo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...