Thursday, June 10, 2010

MISS DAR INDIAN OCEAN KUPATIKANA LEO


picha na www.fullshangwe.blogspot.com

Shindano la Miss Dar Indian Ocean ambalo liko chini ya maandalizi ya Frontline Management limepangwa kufanyika wiki hii tarehe 10 juni katika hoteli Double Tree Hilton.
Mpaka sasa kambi ya Miss Dar India Ocean ina wasichana 12 ambao ni Irene Haule (20), Jacqueline Madundo (20), Esthet Flavian (20), Rose Masanja (22), Nurie Ahmed (18), Ramla Mohamed (19), Happy Whitney Andrew (19), Edna Kwilasa (22), Irene Hezron (22), Winnie Richard (20), Aneth Brayson (23), Rehema Faraji (22), Magreth Hussein (18) and Alice Lushiku (23).
Kambi hii ilianza tarehe 2 Juni na imehusisha shughuli mbali mbali kama mafunzo ya uvaaji, kujiremba, HIV/AIDS, ushauri nasaha, uongozi, unadhifu na maswala ya jamii.
Vile vile warembo wa kitongoji hiki wanatarajia kutembelea kituo cha watoto yatima cha Mitindo House ambako watapaka kituo hiki rangi kwa hisani ya Robiallac.
Mshindi wa Dar Indian Ocean atapata Tshs. Million 1.2, ikifuatiwa na Laki 8 kwa mshindi wa pili, laki 5 kwa mshindi wa tatu na laki moja moja kwa washindani waliobaki.
Shindano hili limedhaminiwa na Vodacom, Redds, Robiallac na Shear Illusion, na tiketi zanapatikana kwenye maduka yote ya Shear Illusion na kwenye ofisi za Frontline Management zilizopo Kinondoni kwa Tshs. 30,000 tu.
Nancy Sumari, meneja wa matukio kwenye kampuni ya Frontline Management amesema “nia kubwa sana ya kujihusisha kwenye uandaaji wa mashindano haya ya Miss Tanzania ni kuhakikisha kwamba washiriki wanapewa mwongozo utakaowawezesha kumudu presha zinazowakumba wanaposhinda taji. .

No comments:

Post a Comment