Mrembo wa Pangani kupatikana Juni 4
|
benedict kaguo
Na Benedict Kaguo,Pangani
MASHINDANO la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Pangani linatarajiwa kufanya juni 4 mwaka huu katika ukumbi wa Safari Lodge Annex mjini humo.
Mkurugenzi wa MO entertainment,Mohamed Hamie 'Anko Mo' ambao ndio waandaji wa mashindano hayo alisema jana kuwa hadi sasa jumla ya warembo nane wameshajitokeza na wako kwenye maandalizi ya mwisho.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,washindi watatu wataoshinda watapata nafasi ya kushiriki Mashindano ya Miss Tanga yanayotarajiwa kufanyika Juni 19 mwaka huu.
Aliwataja warembo hao kuwa ni Asha Athumani, Aziza Halifa, Mwajuma Ally, Nuru Hamisi, Hadija Issa, Mwanahamisi Rashid, Barki Amir, na Agnes Sambo.
Mashindano hayo ya Miss Pangani 2010 yamedhaminiwa na Mwekasu Hostel, Sofia Production, Breeze Fm, Pangani Coast Cultural Tourism Programme, Salome Hair Dressing Sallon na VodaCom Tanzania.
No comments:
Post a Comment