Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 4, 2010

VIONGOZI WA MCHEZO WA POOL WANAUWA MCHEZO HUOO TANGA

Viongozi wanaua mchezo wa Pool Tanga


Na Oscar Assenga,Tanga.

Baada ya wiki ya jana kuangalia suala zima la mchezo wa mpira wa miguu mkoani hapa hebu leo tuangalie mchezo Pool Table ambao kwa hivi sasa unaonekana kuwa na kasi sana hapa nchini kwa kupendwa na vijana wa rika zote na kujipatia umaarufu mkubwa sana.

Nataka kuelezea mtazamo wangu kuhusu mchezo huu ambao unaonekana kama kutokuwa na muelekeo kutokana na viongozi wake mkoani hapa kuwa wabinafsi.

Kilichonipelekea kuandika mtazamo huu ni kutokana na kile kinachoonekana wakati wa mashindano hayo ambayo huwa yanafanyika katika mikoa mbalimbali hapa nchini lakini katika mkoa huu inasemekana kuwa gharama za mashindano ya mchezo huo ambazo zinatolewa na wadhamini wa michuano hiyo kampuni ya bia hapa nchini kupitia bia yake ya Safari Lager huwa haziwafikii walengwa wanaoshiriki mashindano hayo licha ya fungu kwa ajili ya mchezo huo kutolewa.

Aidha wakati mwengine fedha za ushiriki wa michuano hiyo kwa wachezaji huwa zinatolewa na wadhamini lakini cha kushangaza vingozi hao wanashindwa kuzifikisha kwa walengwa wa mchezo huo na wakati mwengine ziwafikie walengwa zikiwa pungufu.

Je kwa staili hii tutafika kweli kwa njia hizi ambazo ni kama kukatishana tamaa katika harakati za kuuletea mchezo huo maendeleo mkoani hapa? Mchezo ambao unaonekana kuwa na mashabiki wengi na kupendwa sana.

Mchezo huo ambao ulianza kuwa na kuvutia mashabiki wake mkoani hapa 2008 na kuonekana ni mchezo ambao unapendwa kama ulivyo mchezo wa soka.

Na je kwa staili hii ya viongozi wa mchezo huo kuonekana wababaishaji kweli tutafika au ndio kusema uswahili wetu tunauingiza mpaka katika michezo.

Mara nyingi wachezaji wa mchezo huo wamekuwa
wakiwalalamikia viongozi wao kutokana na viongozi hao
kutokuwa wazi kwa kuwaeleza wachezaji kanuni na taratibu za mashindano ya mchezo huo hali inayowafanya wachezaji hao wakati mwengine kunyanganywa pointi wakati wa mashindano hayo bila kujua kanuni na taratibu za mchezo huo.

Katika mashindano mbalimbali ya mchezo huo yaliyofanyika mkoani hapa mwaka jana tulibahatika kutoa timu nane kushiriki katika michuano ya kitaifa kwa kuchuana na hatimaye kupatikana timu moja ambayo ilikwenda kushiriki mkoani Mbeya na kufanya vizuri.

Sasa viongozi hao na wachezaji kutokuonyesha ushirikiano kweli tutafika ?Jitihada za hali ya juu zisipofanyika ipo hatari ya mchezo huo kupotea kabisa hapa nyumbani kutokana na kuwa na viongozi ambao ni wababaishaji.

Kama kweli wadau mchezo huo tunataka kuuinua katika
mikoa mbalimbali hapa nchini ni lazima wadhamini wa
mchezo huo (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager wafanye ziara za kutembelea vilabu vilabu mchezo huo mikoani ili kuweza kuja changamoto zinazokuwa zikiwakabili kabla ya kuanza kwa mashindano.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...