Mwanadada Serena William aliyekuwa na uhusiano na mwanamuziki/ muigizaji Common wameripotiwa kutengana.
Nyota huyu wa tennis aliyekuwa kwenye uhusiano wa miaka miwili na rapa Common, hawako pamoja tena.
Sababu za kutengana kwao mpaka sasa hazijajulikana ingawa april mwaka huu wawili hawa walionekana pamoja.
Cha kushangaza ni kwamba wakati wa uzinduzi wa filamu yake "Just Wright" , Common aliambatana na mama yake kwenye sherehe hizo.
Mapema wiki hii alipokuwa kweney kipindi cha mahojiano cha Ellen DeGeneres, Common alikiri kuwa anatamani kufunga ndoa na kuanza familia lakini hakumzungumzia Serena hata kidogo.
No comments:
Post a Comment