Marquee
tangazo
Tuesday, August 3, 2010
JUMA NATURE ASEMA MADJS WANAMBANIA
Juma Nature
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Juma Kassim 'Nature' amesema yeye na kundi lake bado wapo juu kimuziki lakini wanabaniwa na baadhi ya madj wa vituo vya redio nchini kwa kutopiga nyimbo zao.
Nature aliyasema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni mwishoni mwa wiki ambapo alisema kuwa nyimbo walizonazo ni nzuri na zinauwezo wa kuzishinda nyimbo nyingi zilizopo juu, tatizo ni baadhi ya madj wamekuwa hawataki kuzicheza.
Alisema yeye anakawaida ya kutotaka kupelekwa na mtu yeyote kwa ajiri ya maslahi yake hivyo yawezekana kuna watu ambao wanampikia majungu ili awe chini jambo ambalo yeye anasema hawataweza.
Nature alisema kutokana na uwezo alionao yeye anaamini kuliteka soko la muziki huo nchini ni vyepesi iwapo angepata ushirikiano wa kutosha kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
"Wanabana sana lakini kwenye ukweli pataonekana kwani huwezi amini nyimbo tulizonazo lazima usimame, cha kushangaza zinapewa kipaumbele nyimbo za ajabu za ukweli wanaziacha," alisema Nature.
AKizungumzia kuhusu kundi la Tmk kuvunjika mara kwa mara alisema yeye na wenzake waliobaki katika kundi lake ndio Temeke asilia, lakini wengi waliokuwemo awali walikuwa ni wakuja.
Nature alisema yeye wakiwemo kina Mabaga Fresh, Inspector ndio Tmk wenyewe hao wengine wote walikuwa wakipokelewa tu na baadaye wakawa vibuli wakati walikuwa wakila kwa mgongo wa mtu mmoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment