Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 2, 2010

Shamba la Bibi latua na Stahili za Ngosha Mosha na Mbasha Wasome Wameahaishwa vipi !!!




Ni kava la kitabu kipya cha katuni kilichochorwa na Bashir Adams
'Mors'. Kimetolewa na kusambazwa na Bantu Entertainment Ltd. chini ya
mkurugenzi wake Marco Tibasima. Kitapatikana mitaani kuanzia Jumatatu
tarehe 2 Agosti, 2010 kwa bei ya tsh. 3000/- tu. Kwa maelezo zaidi jinsi
ya kukipata 0765927833.


Marco Tibasima
Artist/Graphic Designer
PO Box 9974
Dar es Salaam, Tanzania
tel: +255 754 308221 (in Tanzania)
tel: +256 756 417507 (in Uganda)
webpage: www.raisingvoices.org/marco.php

Wasifu wa Mchoraji wa Shamba la Pesa
Bashir Adams a.k.a Mors alizaliwa mwaka 1985 huko Ngarenaro, jijini
Arusha. Alianza elimu ya msingi Ngarenaro Shule ya Msingi Mwaka 1994 hadi
mwaka 2000. Elimu ya sekondari alisoma Kaloleni Shule ya Sekondari kuanzia
mwaka 2001 hadi 2003, kisha akamalizia Temboni Shule ya Sekondari ya
jijini Dar es Salaam mnamo mwaka 2005.

Alianza kupenda uchoraji alipokuwa na miaka minne tu baada ya kumwona
kijana mmoja wa rika lake waliyeishi naye mtaa mmoja aliyeitwa Yassini
akichora picha mbalimbali zilizomvutia. Pia alipata hamasa kutoka kwa dada
yake aitwaye Hidaya Adams ambaye Bashir anakiri alikuwa akichora picha
ambazo zilimpa hamu ya yeye kujifunza pia. Bashir aliweza kwa nyakati
tofauti kuwakilisha shule yake ya Ngarenaro kwenye mashindano mbalimbali
ya uchoraji Mkoani Arusha na kushinda zawadi kadhaa.

Kazi zake zilianza kuonekana rasmi kwenye jarida la Bantu mwaka 2007 na
baadaye gazeti la Ambha.

SHAMBA LA PESA ni kitabu chake cha kwanza na anatarajia kuendelea kutoa
mfululizo wa mikasa hii ya Ngosha, Mosha na Mbasha.

Hakusita kuwashukuru wafuatao katika safari yake ya kufikia mafanikio haya
ambao ni: Marco Tibasima wa Bantu Entertainment Ltd, Nicolaus Munga
‘Nicoman’ wa Arusha, Karim Swago ‘Kakakeri’, Abubakary Mustapha ‘Mandelaa’
na Abedi K. Kimolo wa Ngarenaro, Arusha na Francis John wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.

Anapatikana kwa simu: 0754 546964 / 0658 546964.
Baruapepe: mossadam@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...