
Show zilianzishwa na wasanii mbalimbali kutumbuiza, wengine wakashangiliwa na wengine kuzomewa kwa Sauti kubwa ya umati, ktk walioshangiliwa na kuzomewa wapo wasanii wawili zaidi Bushoke na Izzo B ambao makelele waliyopigiwa yana maana kubwa sana na hayatakiwi kupuuzwa kabisa!
Bushoke alizomewa sana pale alipoanza kuifagilia serikali eti imefanya mambo mazuri mengi sana, umati mkubwa wa vijana ukapinga ktk staili hio
Izzo B ndie aliyeshangiliwa sana zaidi alipoimba kile kibao chake cha "RIZ ONE Ongea na Msure" nyimbo inayomwelekeza Riz aongee na mkubwa juu ya mambo ya serikali ambayo mengi hayajakaa sawa! pia alipotaka umati uzomee TANESCO, umati ulizomea saaaaana!




No comments:
Post a Comment