MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala
amekanusha taarifa zilizozagaa mitaani kuwa halmashauri hiyo imesimamisha
mikataba ya mgambo wa wilaya hiyo na kuingia mkataba na Kampuni binafsi ambayo
ingeanza kazi Mei Mosi mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa wilaya
hiyo, Gabriel Fuime wakati alipokuwa akizungumza na Fullshangweblog jijini Dar es Salaaam jana kuhusu
uvumi huo kuwa hauna ukweli wowote.
Alisema Halmashauri haijafikia uamuzi huo
bali kinachofanyika hivi sasa ni kuangalia nama iliobora katika usimamizi
wakazi zinazofanywa na mgambo hao ambapo kama kutakuwa na ulazima kazi hiyo
watakabidhiwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
“Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi
kuwa jeshi la mgambo halitendi kazi zake kwa kufuata sheria kwamba wamekuwa
wakijihusisha zaidi na vitendo vya rushwa”alisema Fuime
Fuimea alisema ndio maana wamo katika
upembuzi yakinifu ili ikiwezekana wawape jeshi kazi hiyo kwa kuamini kuwa
wataifanya katika kiwango bora ukilinganisha na hivi sasa.
Alisema vikao kuhusu mipango ya kuboresha
huduma hiyo vinafanyika na wakati ukifika itatolewa hadharani na kila mmoja
wenu atajua lakini kwa sasa hatujawasimamisha mgambo hao ambapo wanaendelea na
kazi kama kawaida.
Aidha, mgambo hao wamekuwa wakifanyakazi kwa
mkataba wa miezi mitatu ambapo mara wamalizapo huomba mkataba tena bila ya kuwa
na uhakika wakufanikiwa.
Fuime alisema mgambo hao hulipwa posho ya
ujira kwa siku ndani ya mwezi mmoja kiasi cha shilingi 120,000.
No comments:
Post a Comment