Bingwa wa
mchezo wa pool mmoja mmoja(singles) Mkoa wa Shinyanga, Ndala Ndefu akicheza
dhidi ya mpinzani wake Majaliwa Cyipilian wakati wa mashindano Safari Pool
Taifa ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika
Klabu ya Garden mwishoni mwa wiki.
Na Michael Machellah;
MIKOA mitano
kati ya 16 inayoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mikoa
imekamilisha fainali za ke mwishoni mwa wiki hii kwa kupata klabu,mchezaji
mmoja mmoja (single) wa kiume na kike.
Katika
mashindano hayo yalihudhuriwa na wageni rasmi mabalimbali kila Mkoa ambao pia
waligawa zawadi kwa washindi.Mshindi wa kwanza alijinyakulia Shilingi laki
saba, mshindi wa kwanza wa kiume alipata shilingi laki tatu nusu na wa kike
laki mbili na nusu pamoja na zawadi zingine kwa washindi wa pili na tatu.
Mkoa wa
Shinyanga mabingwa ni Klabu ya New Stand, mchezaji wa single wanaume ni Ndala
Ndefu na singles wanawake ni Sada Tuwa, Mkoa wa Kagera mshindi wa timu ni klabu
ya Balele,singles wanaume ni Hakimu
Mzamili na singels wanawake ni Angel Mfaume
Tabora
mabingwa ni Klabu ya Texas, singles wanaume ni Waziri Ally na singles wanawake
ni Angel Mfaume wakati Manyara mabingwa ni Klabu ya Janja Wild, singles wanaume
ni Ally Nada na singles wanawake ni Chiku Mohamed.
Kilimanjaro
mabingwa ni klabu ya Mbosho,singles wanaume ni Teter George na singles wanawake
ni Cecilia Kileo.
Washindi
hawa watawakilisha mikoa yao katika mashindano ya Taifa ambayo yanatarajiwa
kuanza kutimua vumbi Semptemba jijini Mwanza kwa kushilikisha Mikoa 16 ya
Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment