Saturday, August 18, 2012

RAIS KIKWETE ALIPOTETA NA RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Malawi Mh Joyce Banda nchini Msumbiji, ambapo wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za Kidiplomasia kupititia Kamati Maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo (Picha na Freddy Maro).

MAPUTO, Msumbiji

RIS Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na mwenzake wa Malawi, Joyce Banda, wamekutana nchini Msumbiji na kufanya mazungumzo mafupi yenye nia ya kumaliza mgogoro wa mpaka unaohusisha nchi zao.

Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Joyce Banda walikubaliana kumaliza mgogoro huo Kidiplomasia, kupititia Kamati Maalumu iliyoundwa kushughulikia sakata hilo linalohusu mpaka sehemu ya Ziwa Nyasa.

Kupitia mazungumzo hayo, Rais Kikwete alisema: "Mimi ndiye Amir wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, sijapanga wala kutoa agizo la vita...

"Wanasiasa na waandishi wa habari wa mataifa yote mawili, wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki na chokochoko miongoni mwa raia, hasa wa maeneo ya mpakani.

Rais Kikwete akaenda mbali zaidi kwa kutaka: "Watanzania na Wamalawi, muyapuuze maneno hayo, badala yake acheni Diplomasia ifanye kazi yake,"

No comments:

Post a Comment