Mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) kutoka nchini Brazil Roberto Azevedo (katikati) akijadiliana jambo na Balozi wa Brazil Francisco Luz. |
MGOMBEA wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Biashara la Kimataifa (WTO) Roberto Azevedo kutoka nchini Brazil
amekamilisha kampeniyake hapa nchini leo kwa kuitaka Tanzania imuunge Mkono
kwenye kiti hicho kutokana na mipango yake kwa nchi zinazoendelea.
Akizungumza na waandishi wabari jijini Dar es Salaam
leo Azevedo amesema anaitaka Tanzania imuunge mkono kwenye upigaji wa kura
kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho hadi sasa wagombea tisa kutoka nchi
mbalimbali wamejitokeza..
Kaabla ya kukutana na waandishi wa habari mgombea
huyo alikutana na Waziri wa Mambo ya Nnje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad
Membe na kumueleza malengo na mikakati yake kwenye nafasi hiyo na kwanini
Tanzania imuunge mkono.
Aidha Azevedo alisema tatizo la msingi kwa shirika
hilo kwa sasa ni kutotoa hamasa kwa nchi mbalimbali juu ya mambo mbalimbali ya
shirika hilo, lakini pia kutokuwepo kwa ushirikishwaji wan chi zinazoendelea
wakati wa uanzishwaji wa shirika hilo mara baada ya vita ya pili ya dunia.
“Nitahakikisha mawazo ya nchi zinazoendelea
yanafanyiwa kazi kwa manufaa ya shirika hilo na wanachamawake.”
No comments:
Post a Comment