Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 5, 2013

MVUA KIDOGO MAJI KIBAO! Hili ndilo jiji la Dar tena eneo la Posta!



Mwendesha pikipiki akikatiza kwenye moja ya mitaa ya eneo la Psta jijini Dar es Salaam ambao umefurika maji kufuatia mvua zalizonyesha kwa muda mfupi nakusababisha baadhi ya mitaa kufunga na watu kushindwa kupita.

 

Eneo la Posta barabara ya Jamuhuri  ubavuni mwa jengo la Supermarketi ya Imaraseko likiwa limefurika maji kufuatia kunyesha mvua kwa muda mfupi hali iliyosababisha usumbufu kwa watumiaji wa eneo hilo.
Watu mbalimbali wakipita kwenye dimbwi hilo la maji kwa kukanyaga juu ya kreti tupu za kuhifadhia Soda baada ya wajasiriamali kuziweka na kuwalipisha shilingi miamoja kwa kila mtu.
Kazi kwelikweli vijana wabunifu!
Mmoja wa vijana hao akiwazuia watu ili aweke vizuri vifaa vya kuvukia.
Magari nayo yalionja karaha ya mvua!
Eneo la Kariakoo nalo lilikumbwa na uhaba wa magari kutokana na mvua hiyo kusababisha magari mengi kuharibika na abiria kurundikana kwenye vituo vya mabasi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...