Katika
hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na
umri wa miaka mitano jana usiku alivamia ndani ya uwanja wakati Brazil
ilipokuwa ikimenyana na Afrika Kusini na kwenda moja kwa moja kwa
mshambuliaji Neymar wa Brazil. Katika kuonyesha furaha ya kufuatwa na
mchezaji huyo, Neymar aliamua kumkumbatia na kisha wachezaji wote wa
Brazil waliamua kumbeba juu. Katika mechi hiyo, Brazil iliinyuka Afrika
Kusini mabao 5-0.
No comments:
Post a Comment