Friday, March 7, 2014

MTOTO AVAMIA UWANJANI SAUZI, AMKIMBILIA NEYMAR


Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitano jana usiku alivamia ndani ya uwanja wakati Brazil ilipokuwa ikimenyana na Afrika Kusini na kwenda moja kwa moja kwa mshambuliaji Neymar wa Brazil. Katika kuonyesha furaha ya kufuatwa na mchezaji huyo, Neymar aliamua kumkumbatia na kisha wachezaji wote wa Brazil waliamua kumbeba juu. Katika mechi hiyo, Brazil iliinyuka Afrika Kusini mabao 5-0.

No comments:

Post a Comment