Mkuu
wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga (katika) akiongozana na Mkuu wa
Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba
Mwekundu ”Red Cross” Mkoa wa Mbeya, Bw. Ulimboka Mwakilili, wakikagua maeneo
yaliyoathirika na Mafuriko wakati walipokwenda kukabidhi msaada wenye thamani ya
Shilingi Milion 10 kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga (kulia), akipokea msaada wa vyandarua
kupitia Chama cha Msalaba Mwekundu ”Redcross” kwa niaba ya wahanga wa mafuriko
wa wilaya hiyo toka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule
(kushoto), pamoja na Mkuu wa Vodacom Tanzania Nyanda za Juu Kusini, Bw. Macfyden
Minja (katikati). Msaada wa jumla ya shilingi Milioni 10 kwa misaada mbalimbali
kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga (kulia) akipokea msaada wa vyandarua
kupitia chama cha Msalaba Mwekundu”Redcross”kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wa
wilaya hiyo, toka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania Nyanda za Juu Kusini, Bw.
Macfyden Minja. Anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya
Mwakifulefule. Jumla ya shilingi Milioni 10, zimetumika kwa misaada mbalimbali
kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu
wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, akizungumza na baadhi ya wanafunzi
wa Shule ya Msingi Kajunjumele iliyopo wilayani Kyela, iliyoathiriwa na mafuriko
yaliyotokea hivi karibuni, alipotembelea shule hiyo, mara baada ya kukabidhi
misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Mkuu wa Wilaya hiyo
(hayupo pichani),kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wilayani humo.
Mkuu
wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, akiingia kwenye moja ya darasa
lililoathirika na mafuriko hivi karibuni katika Shule ya Msingi Kajunjumele,
iliyopo Wilaya ya Kyela, alipotembelea shule hiyo, mara baada ya kukabidhi
misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Mkuu wa Wilaya hiyo
(hayupo pichani), kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wilayani humo. (Picha zote na
mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment