Habari
wadau, Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS),
kimeandaa mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari za michezo chipukizi
wa umri kati ya miaka 19-25 yatakayofanyika Doha Qatar mwishoni mwa
mwaka huu wakati wa mashindano ya Dunia ya Mchezo wa Kuogelea.
Kutokana na hali hiyo, AIPS imetoa nafasi chache kwa watakaokidhi
vigezo vyao katika mabara mbalimbali duniani. Hivyo nimeattach barua yao
na nini kinatakiwa katika mafunzo hayo, ambayo wahusika watagharamia
nauli ya kwenda Doha na kurudi mji husika anaotoka mhusika, chakula na
malazi muda wote atakaokuwa huko.
Kwa vile hatua ya mwisho itahusisha chama
cha nchi husika kumthibitisha muombaji, naomba wote watakaofikiri wana
sifa zinazotakiwa wasome vizuri hiyo attachment, kisha watume kwa Makamu Mwenyekiti TASWA, Egbert Mkoko ambaye ndiye atasimamia jambo hilo kwa email: njali5@yahoo.com nataswatz@yahoo.com
Lakini
pia kama utamudu unaweza ukaomba binafsi bila kutumia chama na mwisho
wa kufanya hivyo ni Agosti 15 mwaka huu na watume kwa
email:youngreporters@aipsmedia.com. Kwa watakaotaka kupitia TASWA
wajitahidi kabla ya Agosti 10 mwaka huu.
Tusihofie
kuomba kwani mwaka 2011 aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Mtanzania mwenzetu, Mwita Mwaikenda aliomba nafasi hiyo na
aliipata. Ukiwa unahitaji ufafanuzi tuwasiliane 0713-415346.
Nawasilisha,
Katibu Mkuu TASWA
No comments:
Post a Comment