Promotor
wa mbambano wa ngumi za usiokuwa na ubingwa, Rashid Kipanga
akiwatambulisha, Manenono Osward(Mtambo wa Gongo) kulia na Abdalah
Pazi(Mudi Mbabe) wanaotarajia kuchuana Augosti 10,2014.Makubaliano hayo
yalifanyika katika Ukumbi wa Mwinjuma Dar es Salaam.
Na Mwandioshi Wetu.
BONDIA
Mkongwe wa masumbwi, Maneno Osward maarufu kwa jina la “Mtambo wa
gongo” jana amesaini rasmi kuzichapa na bondia chipukizi Abdalah Pazi
maarufu kwa jina la “Dula Mbabe”.
Maneno
Osward (Mtambo wa Gongo) alisaini jana huku akimtahadhalisha mpinzani
wake kuwa yeye hachagui umri,bali mtu yeyeto ambaye yuko tayari na
vigezo vimezingatiwa vya Chama cha Ngumi nchini yeye yuko tayari muda
wote.
Mtambo
wa gongo wa Gongo alitamba kuwa kijana bondia chipukizi anayejiita Mudi
Mbabe anataka kumbadilisha jina na kuwa Mudi mnyonge na katika raundi 6
zilizopangwa hatafika mwisho.
Nae
Abdalah Pazi bondia chipukizi alitamba yeye hataki ngojela
atakachokifanya kwa anayejiita mkongwe wa masumbwi kitakuwa historia
katika maisha yake kwani hatafika raundi ya nne.
Mwisho
Mudi aliwataka wapenzi na mashabiki wa Ngumi kujitokeza kwa wingi
hususani madereva bodaboda ambao ndio wafanyakazi wenzake wajitokeze kwa
wingi kumshangilia atakavyomfanya vibaya Maneno Osward (Mtambo wa
Gongo) na kumbadilisha jina kuwa Mtungi wa maji.
Mbambano
wa Maneno Osward(Mtambo wa Gongo) na Abdalah Pazi(Mudi Mbabe)
umedhibitishwa na Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TBBC), Chaurembo
Palasa ambaye aliwataka mabondia wasiwe chanzo cha fujo katika mpambano
huo ikiwa ni kukuza na kuendeleza mchezo wa Ngumi nchini.
Mpambano
huo utakuwa ni wa KG 78-Super middle weight utakaofanyika katika ukumbi
wa CCM Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam tarehe Augosti
10,2014 kuanzia saa kumi na mbili.
Wasanii
watakaotoa burudani katika mbambano huo ni Kikosi cha Mizinga chini ya
Uongozi wa Karapina,Sster P pamoja na wengine wengi.
Mgeni rasmi katika mbambano huo ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge.
Mchezaji
wa Nngumi, Maneno Osward(Mtambo wa Gongo) akisaini mkataba wa kupigana
na Abadalah Pazi(Dula Mbabe) Augosti 10,2014 katika Ukumi wa CCM
Mwinjuma jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Chama cha Ngumi
Tanzania(TPBC), Chaurembo Palasa akishuhudia
No comments:
Post a Comment