Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota akionesha tuzo ya ushindi katika sekta ya mawasiliano.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
Muonekano wa Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.Baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya
Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya
kutwaa tuzo hiyo katika sekta ya Mawasiliano.Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba.
KAMPUNI
ya Simu Tanzania, TTCL imeshinda tuzo katika kundi la kampuni zinazotoa
huduma za mawasiliano, kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Sabasaba
yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Peter Ngota katika
uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es
Salaam yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Ushindi
wa TTCL unatokana na ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo
katika upande wa mawasiliano ya simu na pia mawasiliano ya intaneti
"DATA". TTCL imesema ushindi huo umeipa hamasa ya kuendelea kubuni
bidhaa ambazo zitakuwa chachu ya ukuaji uchumi nchini.
No comments:
Post a Comment