Magwiji wa muziki wa dansi nchini, Msondo
Ngoma na Mlimani Park Orchestra “Sikinde” siku ya Iddi Mosi watachuana vikali
katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo wa Nani Mtani Jembe ni kwa
ajili ya kusherehekea sikukuu ya Id El Fitr na pia litaamua ni bendi ipi kali kati
yao.Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga
amesema pambano hilo litaanza saa nane alasiri hadi majogoo.
Kapinga alisema bendi zote mbili ziko msituni
kujiandaa na mpambano huo.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga
kwenye jukwaa lake ili kulinda upinzani wao.
Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera alisema jana watapiga nyimbo
zao zote kali ili kuhakikisha wanaisambaratisha Sikinde.
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban
Dede, Mabera, Eddo Sanga, Juma Katundu,
Roman Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi.Naye
kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
“Tuna
waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Baadhi
ya wanamuziki wanaounda Sikinde ni Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Abdala
Hemba, Musemba Waminyugu.
Ramadhani
Mapesa, Adofth Mbinga, Kelvin Mausi Mjusi Shemboza, Tonny Karama, Bonny Bass,
Habibu Abass Jeff , Juma, Juma Choka, Mbaraka Othman, Hamisi Mirambo, Ali
Yahaya, Yusuph Benard na Ali Jamwaka.Pambano
imedhaminiwa na Konyagi na
Saluti5.
No comments:
Post a Comment