Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 5, 2010

STANDARD CHARTERED YAZINDUA KADI MPYA YA KIPEKEE




Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Banki ya Standard Chartered Bw. Tirus Mwithiga (kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Jeremy Awori (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kipekee wa ,Bi. Masala Korosso, wakiwa wameshika mfano wa Card mpya ya VISA Infinite itakayokuwa inatumiwa na wateja wa benki hiyo kupata huduma popote watakapokuwa. Uzinduzi huo ulifanyikanyika Makao Makuu ya Benki Dar es Salaam

BENKI ya Standard Chartered huduma mpya ya Priority Banking ya kutumia kadi aina ya Visa Infinite inayowezesha wateja wake kupata huduma popote yalipo matawi ya benki hiyo duniani.

Uzinduzi wa huduma hiyo mpya ulizinduliwa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Bw. Tirus Mwithinga alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema huduma hiyo inawalenga wateja wa kipato cha juu kwa lengo la kuwawezesha kupata mahitaji ya kibenki popote wanapokuwa nje
"Faida ya huduma hii ni kuwawezesha kupata huduma popote katika nchi 20 ambapo benki yetu ina matawi yake," alisema Bw.Mwithinga.

Alisema ili mteja aweze kupata huduma hizo hatakiwi kutoa gharama za nyongeza zaidi ya kutakiwa kufikia vigezo vilivyowekwa . "Mteja akishakidhi vigezo vilivyowekwa hatahitaji kulipia gharaza zozote,

Alisema matawi ya benki hiyo kuanzia sasa yatakuwa na eneo maalum la kutoa huduma za Priority Benking ili kuwawezesha wateja kujiunga. Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Jeremy Awori alisema hiyo ni huduma ya kwanza kutolewa na benki za hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...