Wachezaji
wa timu za waendesha Bodaboda kutoka Tegeta na Kawe, wakichuana kuwania
mpira wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Bodaboda 'Bodaboda
Cup' inayoendeshwa na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
Katika mchezo huo timu ya Kawe imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya
Tegeta, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Tanganyika Pakers Kawe
jijini Dar es salaam leo.
Mashindano
hayo yanashirikisha timu za mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ambazo
zinatoka katika maeneo ya Kimara, Kawe, Tegeta, Mabibo na Ubungo, ambapo
wachezaji washiriki wa mashindano hayo wanatakiwa kuwa ni waendesha
pikipiki za kupakia abiria tu 'Booda'. Awamu ya kwanza ya ligi hiyo
ilikuwa na timu 32 na sasa ni awamu ya pili ambapo timu 16 zinashindana
ili kupata timu 8 zitakazoshiriki Ligi ya Nane Bora na hatimaye kupata
mshindi wa mashindano hayo ya 'Kinondoni Bodaboda Cup'.
Lengo
la Mashindano hayo ni kuwakutanisha waendesha Bodaboda wote wa mkoa wa
kipolisi wa Kinondoni ili waweze kufahamiana wao kwa wao, lakini pia
ili jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani liweze kuwaelimisha
juu ya sheria za usalama Barabarani na Ulinzi Shirikishi kwa jamii.
No comments:
Post a Comment