Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania,Teddy Mapunda wa tatu kutoka (kulia) akimkabidhi mpira Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA - Nakayama iliyopo Rufiji, mkoani Pwani Rehema Mshama(kulia) ikiwa ni mchango wake katikakuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ili waweze kujiendeleza katika sekta ya michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), jijini Dares Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania, Teddy Mapunda wa nne kutoka (kushoto ) akimkabidhi mpira Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama iliyopo Rufiji, Mbwana R. Mbwana wa tatu kutoka (kulia) ikiwa ni mchango wak katika kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ili waweze kujiendeleza katika sekta ya michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), jijini Dares Salaam.
Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Sekondari ya Wama Nakayama iliyopo Rufiji, Mbwana R. Mbwana wa tatu kutoka (kulia) na wanafunzi wa shule hiyo wakifurahia vifaa vya michezo baada wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania, Teddy Mapunda kutoa mchango huo ili kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika sekta ya michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), jijini Dares Salaam. Picha zote na Magreth Kinabo -maelezo.
****************************************
****************************************
Na Anna Nkinda – Maelezo
Wadau
wa michezo, wapenzi wa amani, afya na maendeleo ya vijana nchini
wameshauriwa kuwekeza zaidi katika michezo kwani inafaida kubwa katika
maisha ya mtoto kwa kuwa inamuepusha na vishawishi vingi vya afya ya
uzazi.
Ushauri
huo umetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) Daud Nasib wakati akiishukuru Kampuni ya Montage
Tanzania kwa kutoa vifaa vya michezo kwa ajili ya shule ya Sekondari
ya wasichana ya WAMA- Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani.
Nasibu
alisema kama wadau hao watahitaji kupata msaada wa kuzitambua shule
zenye mahitajia maalum kama ya WAMA- Nakayama watawasaidia kuzitambua
shule hizo.
Alisema
mchango huo ni mzuri kwani unahamasisha umuhimu wa michezo shuleni kwa
kuwa michezo ni muhimu kwa afya ya akili na humuwezesha kijana
kukua vizuri na kwa usalama pale atakapokuwa mwanamichezo
kutamsaidia kujiepusha na mambo mengi yanayoweza kumletea tabu katika
maisha yake.
Akiongea
mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya michezo Teddy Mapunda ambaye
niMkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo alisema wametekeleza yale ambayo
waliyaahidi walipotembelea shule hiyo wakati wa sherehe za sikuku ya Eid
Mubarak alisikia watoto wanapenda kushiriki katika michezo lakini
kulikuwa na upungufu wa vifaa vya michezo na kuamua kuwasaidia vifaa
hivyo.
Teddy
aliwaomba wanafunzi hao kutumia vipindi vya michezo kucheza kwa bidii
kwani michezo ni ajira, uhai na inaongeza akili shuleni pia inaleta
amani na kujenga urafiki na ushirikiano.
Kwa
upande wake Mwalimu wa michezo wa shule hiyo Mbwana R. Mbwana
alishukuru kwa jezi na mipira waliyopewa kwa nia ya kuendeleza michezo
shuleni hapo kwani itawasaidia kushiriki michezo mbalimbali katika ngazi
ya shule na UMISETA.wanakabiliwa na ukosefu wa vuafaa vya michezo
shuleni hapo.
Mwalimu
Mbwana alisema mwaka juzi katika mashindano ya UMISETA walipeleka
wanafunzi saba katika ngazi ya mkoa huko kibaha na mwaka jana walipeleka
wawili ila kupatikana kwa vifaa hivyo anaamini miaka ijayo watapeleka
wanafunzi wengi zaidi na kufanya vizuri zaidi.
Kampuni ya
Montage Tanzania imetoa msaada wa mipira ya kuchezea mpira wa miguu
mitano na pete minne, jezi za mpira wa pete 18 na mpira wa miguu 26 na
jezi za mlinda mlango wa mpira wa miguu mbili.
No comments:
Post a Comment