Meneja Mkuu Uendeshaji wa Benki ya
Posta Tanzania (TPB), Kolimba Tawa (kulia) akimsoma mmoja wa washindi
wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union leo jijini
Dar es Salaam.
Meneja Mkuu Uendeshaji wa Benki ya
Posta Tanzania (TPB), Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza kwa njia
ya simu na mmoja wa washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na
TPB Western Union leo jijini Dar es Salaam akimjulisha ushindi wake.
Mmoja wa vijana maalumu akikabidhi
moja ya kuponi baada ya kuitoa kwenye boksi ili kumpata mmoja wa
washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union.
Mmoja wa vijana maalumu
wakichanganya kuponi kwenye boksi kabla ya kuchagua moja wapo ili
kumpata mshindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western
Union.
Na Joachim Mushi, Dar
BENKI ya Posta Tanzania (TPB)
hatimaye leo imewataja washindi wa droo ya mwisho wa Shindano la
Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union lililokuwa likiendeshwa na
benki hiyo. Akizungumza katika hafla fupi na wanahabari jijini Dar es
Salaam ya kuwataja washindi hao nane, Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB,
Kolimba Tawa alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa benki hiyo katika
kurejesha sehemu ya mapato ya benki kwa wateja wake.
Alisema washindi hao nane kwa
jumla wamejishindia shilingi milioni 1.5. Akifafanua zaidi alisema
mshindi wa kwanza ambaye ni Elias Mwalamala kutoka Dar es Salaam
amejishindia sh. 500,000/-, na mshindi wa pili, Nathan Gawangi kutoka
Kigoma akijipatia kitita cha sh. 300,000/-, huku mshindi wa tatu Bruno
Hindu (Dar es Salaam) akifanikiwa kuibuka na sh. 200,000/-.
Alisema washindi wengine watano
ambao nao benki hiyo itawazawadia sh. 100,000/- kila mmoja ni pamoja na
Miss Farida kutoka Zanzibar, Alfa Mwakalinga wa Dodoma, Mariam Mtungo,
Ramadhan Mapuya kutoka pamoja na Fadhili Daud Mbaga wote kutoka Dar es
Salaam.
Aidha Tawa aliongeza kuwa washindi
wote watapigiwa simu na uongozi wa TPB na kuelekezwa namna ya kupata
zawadi zao waliojishindia wakiwa ni miongoni mwa wateja waliotuma na
kupokea fedha kupitia huduma ya Western Union.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment