Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 2, 2014

MKUU WA MKOA WA PWANI MGENI RASMI TAMASHA LA VYUO –NACTE INTER COLLEGE TANZANIA –DAR ES SALAAM BONANZA.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh, Mwantumu Mahiza siku ya jumamosi wiki hii anatarajia kuongoza Bonanza la Wanavyuo linaloendea sehemu mbali mbali na ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya kaskazini inayoendelea lwemye viwanja mbali mbali chini ya Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd kwa kushirikiana na kituo bora cha Matangazo TIMES FM 100.5.
Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE linatarajiwa kuwa gumzo kwa mkoa wa Pwani kutokana na mfumo wake uliobuniwa kiufundi na waandaaji ambapo timu mbali mbali za Viongozi wa Serikali na zile za mkoa upata fulsa ya kushiriki pamoja kwa kufanya michezo ya soka, kikapu,netball pamoja na Voleyball.

Akizungumzia bonanza la jumamosi Mratibu wa Michezo Vyuoni, Mpalule Shaaban alisema kuwa Mh, Mwantumu anatarajia kufanya Uzinduzi wa Michezo hiyo kwa Mkoa wa Pwani kutokana na kwamba sasa Michezo hiyo itafanyika kila mwaka Sehemu mbali mbali za Tanzania.
"Ni heshima ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wetu wa vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo, kumbuka kwamba michezo hii aijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni"alisema Mpalule.


Sehemu ya pili imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya ustawi wa jamii kijitonyama  tarehe 29/11/2014, ambako Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa dar es salaam, vilicheza katika michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball,katika kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.
sehemu ya kwanza Ilizinduliwa kwenye chuo cha DIT  tarehe 22/11/2014 mwezi huu na kusisimua wengi katika  Michuano lutokana na kuwa na mfumo wa mtoano kuwa kivutio kwa Wachezaji na Mashabiki ambao wengi wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wanaofika kushuhudia michuano hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu.
 Vyuo vilivyokwisha cheza ni  Institute of Adult Education, Institute of Social Work (ISW) - DSM, Lugalo Military Medical School - Dsm, St. Joseph  College (University),  Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ) - DSM, National Institute of Transport (NIT) - DSM, Bandari College - DSM,huku timu mwalikwa ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.
Vyuo vingine ambavyo tayari vimemaliza michezo yao ya awali ni pamoja na IFM ,DIT, CBE, Muhimbili,TRA,  Mlimani Profesianal,na  Royal College, waliokuwa kundi la kwanza lililofanyika viwanja vya chuo cha DIT akiba Posta.
Aidha vyuo vyote vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa kuwahi Viwanjani ili kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano hiyo ya mtoano kuanza na ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa Bonanza na inafanyika kila siku za jumamosi kutokana na wanafunzi kuwa masomoni katika siku za kawaida.

kila mwaka michuano hii itakuwa ikifanyika kwa kushirikisha vyuo mbali mbali  vya elimu ya kati  hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.

Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na  Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.

Wadhamini aliojitokeza mpaka sasa na kuonyesha nia ya kusaidia mashindano hayo ni pamoja na Coca Cola, Vodacom, MLONGE BY MAKAI, CXC –Tours,Bonga Resort & Hoteli, Ikondolelo Hoteli, na 100.5 Times Fm.  
 lakini hata hivyo dirisha la wadhamini bado liko wazi kwa maana bado gharama ni kubwa za uendeshaji ambapo wajitokeze waweze kusaidia michezo hii iliyoanza kwa shamrashamra nyingi na kuwa na mvuto kwa watazamaji ususani wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliojitokeza.

2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...