Makamu
wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland akizungumza jambo na
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Zanzibar, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA),
Patrobas Katambi. Ujumbe wa CHADEMA ukiongozwa na mwanadiplomasia mahiri
Profesa Abdalla Safari, uko nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi
kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa
Safari Abdalla akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP)
Rainer Wieland wakati ujumbe wa CHADEMA ulioko nchini Ubelgiji,
ulipofika ofisi za bunge hilo mjini Brussels kwa ajili ya ziara ya
kikazi. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi,
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa BAWACHA,
Grace Tendega na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri John Mrema.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demoikrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara,
Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum
Mwalimu wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya
(EP), Rainer Wieland, wakati ujumbe wa CHADEMA ulipofika Ofisi za EP
kuanza ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa
Abdalla Jumbe Safari akiwa na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP),
Rainer Wieland, walipokutana jana mjini Brussels, Ubelgiji kwa
mazungumzo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya ujumbe wa CHADEMA
kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
No comments:
Post a Comment