Mchezaji
wa timu ya Makipa wa Tanzania, ambaye ni kipa wa Simba, Ivo Mapunda
(kushoto) akiwania mpira na beki wa Taswa fc, Martine, wakati wa mchezo
wa kirafiki wa timu hizo uliochezwa jana jioni katika uwanja wa Bora
Kijitonyama, maalum kwa ajili uzinduzi rasmi wa Chama cha makipa wa
Tanzania. Katika mchezo huo Taswa fc ilifungwa mabao 3-0.
Kipa wa Yanga, Deogratius Munisi, akijiandaa kupiga mpira huku akifuatwa na mchezaji wa Taswa fc, Moland.
Mchezaji wa Taswa fc, Ibrahim Masoud (kushoto) akiwania mpira na Deogratius Munisi.
Hapiti mtu hapa.........
Beki wa Taswa fc, Sweetbat Lukonge, akimdhibiti Shaban Kado......
Heka heka langoni mwa Taswa fc
Wakati wa mapumziko.......wachezaji wakipata mawaidha kwa mwalimu wao.....
Mapumziko....
Kikosi cha makipa.....
Mabeki wa Taswa fc, Sufianimafoto na Fredy Chuji
, wakishow love baada ya mchezo huo.
WATANZANIA WASHAURIWA
KUITUMIA NEEMA YA GESI KUPELEKA HIFADHI YA JAMII KWA KILA MTU
DSC_0013Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa,na Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya
jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh.
Aggrey Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi
karibuni katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha
(AICC).(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Arusha
MTAALAMU mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo,
ameishauri serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa
wananchi wake.
Dhliwayo alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi
wa jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii
kwa wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka
2025 ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.
Dk. Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa
na Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini
Zimbabwe na Msumbiji.
Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo
makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.
DSC_0005Ofisa anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi.
Usha Mishra akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na
kutoa mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano
uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.
Alisema ipo nchi ambayo ilitumia utajiri wake wa almasi kutengeneza
miundombinu ya barabara na si vibaya kwa Tanzania kutumia utajiri wake
wa gesi kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.
Alisema kama taifa linaweza kuamua asilimia Fulani kutoka katika sekta
ya gesi kuingia katika kuwezesha hifadhi ya jamii ambayo itahakikisha
uwapo wa huduma sawa kwa wote.
Alisema uchumi wa Tanzania kutoka mwaka 2000 hadi sasa umekuwa ukikua
kwa kasi ingawa kasi hiyo haionekani kwa wananchi ambapo wengi
wamejikuta wakiwa katika umaskini wa kukithiri.
Alisema kutokana na tatizo hilo la umaskini wa kukithiri kutoondoka kwa
hali hiyo kunasababisha na sekta husika kutotoa ajira za kutosha ambazo
zingewezesha watu kuneemeka na uchumi unaokua kwa kasi.
DSC_0079Mtaalamu wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo
akitoa mada chokonozi wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi
ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha
ambao umemalizika hivi karibuni jijini Arusha.
Alisema aidha kaya nyingi zimekuwa na idadi kubwa ya watu ikiakisi
umaskini unaoambatana na kaya zenye watu wengi na uzazi wa mapema
unaowakuta wasichana.
Alisema pamoja na mpango mzuri wa serikali kupitia TASAF kupunguza
umaskini wa kukithiri ukishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa,
ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu unawezesha
mipango ya kupunguza umaskini inafanikiwa.
Alisema iwapo TASAF inashughulikia elimu na afya ni dhahiri itahitaji
kuwapo kwa shule na walimu na katika afya hospitali na wauguzi na
madaktari na dawa.” Ni lazima kuwepo na uratibu ili kufanikisha yote
yaliyolengwa” alisema Dhliwayo.
Alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka mataifa ya Rwanda na Eritrea
ambayo yamefanikiwa hifadhi ya jamii eneo la afya kufikia zaidi ya
asilimia 90 huku wakitumia mifumo thabiti ya afya ya jamii kwa kaya.
DSC_0093Kuki Tarimo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitoa mada
chonokonozi wakati wa mkutano huo.
Aidha amesema kwamba mataifa hayo yamefanikiwa katika malengo ya
millennia na kupunguza idadi ya vifo vya wanawake katika uzazi.
Katika mkutano huo ambao uliitishwa na serikali ili kupata misingi ya
utengenezaji wa sera na sheria ili kuwezesha watanzania wote kuwa na
haki katika kei ya taifa kw akuwezeshwa kuondokana na umaskini wa
kukithiri ulihudhuriwa na watalaamu 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Pia ulifunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi
ambaye alisema Tanzania kwa sasa inapojianda kuwa na uchumi wa kipato
cha kati ipo haja ya kuimarisha sekta za hifadhi ya jamii.
DSC_0101Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka
makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster akichangia hoja wakati wa
mkutano huo uliomalizika hivi karibuni.
DSC_0109Meneja Mwendeshaji wa Shirika la Under The Same Sun, Gamariel
Mboya akiuliza swali kuhusiana na serikali imejipangaje katika
kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi wanapataje mafuta ya kuzuia
mionzi ya jua inayopelekea ugonjwa kansa ya ngozi.
DSC_0135Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe,
akijibu swali kuhusiana na serikali imefanya nini kwa walemavu wa ngozi
katika kuhakikisha mafuta kuzuia mionzi ya jua kwa watu hao yanapatikana
kiurahisi ili kupunguza athari za kansa kwa walemavu hao. Kulia ni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
No comments:
Post a Comment