Na Mwandishi wetu
Mwanamitindo
wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika
kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya Diesel na Edun.
Kampeni
hiyo inayoitwa Diesel + Edun ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza
ambapo muanzilishi wa kampuni hiyo, Renzo Rosso - na waanzalishi wa
kampuni ya Edun , Ali Hewson na Bono walisafiri nchi za Uganda na Mali
na kukutana na wakulima wa pamba barani Afrika.
Waanzilishi
hao waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na
pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja.
Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la
Afrika.
Nguo
hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka
mbalimbali nchini Marekani na duniani. Pia nguo za Diesel + Edun
zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Compass Communications Limited, Maria Sarungi
Tsehai amesema kuwa Flaviana ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania
2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika
kushiriki katika kampeni za nguo hizo.
No comments:
Post a Comment