Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(aliyeshika mkasi) akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya
Bwanga – Biharamulo. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John
P. Magufuli na kulia kwa Rais ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj
Eng. Mussa Iyombe. Wengine katika picha ni baadhi ya Mawaziri, Wabunge
na Viongozi wa Mikoa ya Geita na Kagera walioshiriki katika sherehe
hizo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati
wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo.
Lori
aina ya Scania la Kampuni ya MAP CO Ltd. likiwa na usajili namba T 895
AFH/T 226 AGB kama lilivyokutwa eneo la Manyoni mkoani Singida likiwa
limekatika katikati kutokana na kuelemewa na uzito wa mzigo lililoubeba.
-----------------------------
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtaka Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli kuhakikisha
kuwa Sheria ya Usalama Barabarani inasimamiwa vizuri ili kuhakikisha
kuwa barabara zinazojengwa nchini zinadumu kwa muda uliokusudiwa.
Akizungumza
katika eneo la Buziku mkoani Geita wakati akizindua ujenzi wa barabara
ya Bwanga hadi Biharamulo yenye urefu wa kilometa 67, Rais Kikwete
alisema kuwa wizara ya Ujenzi ni lazima ihakikishe inasimamia sheria
zilizopo na hasa hii ya kutoruhusu magari yenye uzito uliozidi viwango
vilivyoainishwa katika Sheria Namba 30 ya Mwaka 1973.
Akisistiza
umuhimu wa kutunza barabara Rais Kikwete alibainisha kuwa “adui wakuu
watatu wanao sababisha barabara kuharibika mapema ni; magari yanayobeba
mizigo zaidi ya uzito uliowekwa kisheria, ujenzi duni usiozingatia
viwango na kuachwa kwa maji kuzagaa barabarani”.
Wakati
huo huo Rais Kikwete alielezea kufurahishwa kwa kuanza ujenzi wa mradi
huo kwani wapo baadhi ya watu waliokuwa waliokuwa wakieneza taarifa kuwa
sehemu hiyo ya barabara haiwezi kujengwa lakini sasa wameumbuka.
Awali
akitoa maelezo ya mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Injinia Patrick
Mfugale alielezea kuwa mradi mradi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa
kiwango cha lami umegharimu Shilingi bilioni 55 fedha zote zikiwa
zimetolewa na Serikali ya Tanzania. “Mradi huu utajengwa kwa muda wa
miezi 27 na hivyo kukamilika mwezi Februari mwaka 2015” alisema Injinia
Mfugale.
Naye
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Magufuli alimhakikishia Rais Kikwete kuwa
wizara yake itahakikisha kuwa inamsimamia mjenzi wa mradi huo ambaye ni
Kampuni ya Sinohydro Ltd. ya kutoka Jamhuri ya Watu wa China ili
aukamilishe kwa muda na viwango vilivyokusudiwa na bila ya visingizio
vya nyongeza ya gharama.
Akimpongeza
Rais kwa kutekeleza ahadi yake, Waziri Magufuli alibainisha kuwa
wananchi wa mikoa ya Geita na Kagera wamefurahishwa sana kuona kuwa
hatimaye barabara hiyo muhimu inajengwa kwani hiyo ndiyo sehemu pekee
iliyokuwa imebaki ikiwa haina lami kwa barabara inayounganisha mikoa
hiyo ya ziwa.Habari kwa hisani ya Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment