Meneja
Msaidizi wa Benki ya Exim, Tawi la Clock Tower Ibrahim Ukwaju
(katikati) akiwaonyesha hundi wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kilakala
iliyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam baada ya wanafunzi
wa shule hiyo kutembelea benki ili kujifunza shughuli na huduma mbali
mbali zitolewazo na benki hiyo.Kushoto ni wanafunzi wa shule hiyo, Eric
Sanga (kushoto) na Mathew Kennedy.
Meneja
Msaidizi Benki ya Exim , Tawi la Clock Tower la Benki ya Exim ya
Tanzania, Ibrahim Ukwaju (kushoto) akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa
shule ya Msingi ya Kilakala iliyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar
es Salaam baada ya wanafunzi wa shule hiyo kutembelea benki ili
kujifunza shughuli na huduma mbali mbali zitolewazo na benki hiyo.
Meneja
Msaidizi Benki ya Exim , Tawi la Clock Tower la Benki ya Exim ya
Tanzania, Ibrahim Ukwaju (mwenye Fulana ya Bluu) akiwaeleza wanafunzi wa
shule ya Msingi ya Kilakala iliyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar
es Salaam jinsi mashine za kutolea fedha (ATM) zinavyofanyakazi baada ya
wanafunzi hao kutembelea benki hiyo jana ili kujifunza shughuli na
huduma mbali mbali zitolewazo na benki hiyo.
Mwandishi Wetu
Benki
ya Exim imetoa changamoto kwa wazazi kuunga mkono tabia ya kuweka akiba
kwa ajili ya watoto ilikujenga jamii yenye uelewa juu ya masuala ya
kifedha katika siku za usoni.
Meneja
msaidizi wa Benki ya Exim ya Tanzania Tawi la Clock Tower Ibrahim
Ukwaju alitoa changamoto hiyo jana wakati wa ziara ya mafunzo ya Shule
ya Msingi ya Kilakala ambayo ipo chini ya uangalizi wa benki hiyo tangu
Agosti 2012 na tayari benki hiyo imesaidia kutatua changamoto mbali
mbali katika shule hiyo zikiwemo za upungufu wa madawati na vitabu.
Matembezi
hayo katika ofisi za benki hiyo yalilenga kuwapatia wanafunzi wa shule
hiyo ya msingi picha halisi ya jinsi gani mabenki yanavyofanyakazi kila
siku na huduma zitolewazo.
Ukwaju
alisema kuwa jamii yenye uelewa juu ya masuala mbali mbali ya kifedha,
hususani vijana ni muhimu katika uchangiaji na ukuaji wa uchumi na
katika mfumo wa fedha wa Tanzania kwa ujumla.
“Inapaswa
wazazi kuwajengea watoto wao tabia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya
maisha yao ya baadae. Ni wakati muafaka sasa kwa wazazi kufungua akaunti
benki kwa ajili ya watoto wao. Jambo zuri ni kwamba benki nyingi nchini
ikiwemo Benki ya Exim zimeanzisha bidhaa zinazolenga watoto moja kwa
moja.” alisema Ukwaju.
Alisema
kuwa Benki ya Exim inamkakati kabambe wa kusimamia na kujenga maendeleo
ya watoto kwa baadae na ndiyo maana benki hiyo ilianzisha kwa makusudi
akaunti maalum ijulikanayo kama ‘Nyota Saving Plan’ kwa ajili ya watoto.
“Akaunti
hii imeanzishwa kwa makusudi kutatua matatizo ya kifedha wanayoyapata
wazazi kama vile kuongezeka kwa gharama za kielimu pamoja na huduma
nyingine muhimu. Ili kupambana na gharama za mfumko wa bei, wazazi
wanahitajika kutunza fedha na kuwekeza, ” aliongeza.
Naye
Mkuu wa shule ya msingi ya Kilakala, Abdul Kutarasa wakati wa hafla
alisema ziara hiyo ya wanafunzi wa shule yake katika benki hiyo ilikuwa
fursa nzuri kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
“Hii
imekuwa ni fursa nzuri ya kujifunza kwa wanafunzi wengi. Naamini fursa
hii itawashawishi wanafunzi kusoma kwa bidii zaidi na tunategemea baadhi
yao sasa wamepata ushawishi wa kufanya kazi kwenye sekta ya kibenki
siku za usoni.
No comments:
Post a Comment