Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MAPAMBANO zaidi ya sita ya ngumi za kulipwa yanatarajiwa kufanyika Ijumaa, wiki hii, katika ukumbi wa Yohana Pub ulioko maeneo ya Msamvu, katika Manispaa ya Morogoro.
MAPAMBANO zaidi ya sita ya ngumi za kulipwa yanatarajiwa kufanyika Ijumaa, wiki hii, katika ukumbi wa Yohana Pub ulioko maeneo ya Msamvu, katika Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na mtandao huu, msemaji wa mapambano hayo ambayo
awali yalipangwa kufanyika Novemba 24 kabla ya kurudishwa nyuma, Mohamed Jeilan
alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba mabondia wote watakaopanda
ulingoni wapo katika mazoezi makali.
Jeilan alisema lengo la mapambano hayo yanayosubiriwa kwa
hamu kubwa mjini Morogoro, ni kuibua vipaji vya mabondia chipukizi na kuendeleza
mchezo huo kiujumla.
Alisema mbali ya mabondia wa Morogoro, mabondia wachache
kutoka jijini Dar es Salaam pia wanatarajiwa kualikwa kwa lengo la kutoa
changamoto katika mapambano hayo.
“Kimsingi maandalizi yanakwenda vizuri na mabondia wote hivi
sasa wanaendelea kujinoa chini ya makocha wao ili kuhakikisha wanafanya vizuri
siku hiyo”, alisema.
Msemaji huyo amewataja baadhi ya mabondia watakaopanda
ulingoni siku hiyo kuwa ni George Masawe ‘G Mawe’, Athuman Dame, Miraji
Abdallah ‘Kinditi One Power’, Salum Saleh ‘Sure Boy’, Beta Kingalu na Ngoda
Stopa.
Jeilan ametoa wito kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi mkoani
hapa kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Ijumaa katika ukumbi huo ili kushuhudia
mapambano hayo.
No comments:
Post a Comment