Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima akiongea na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam wakati wa kumtangaza Athuman Hamisi (kulia)
kuwa Balozi wa Usalama Barabarani kitaifa.
Athumani Hamisi anataraji kuanza kampeni maalum ya kuhamasisha jamii juu ya matumizi sahihi ya vyombo vya usafiri kwa kufanya kampeni hiyo kuanzia mwezi Desemba ambao umeelezwa kuwa na matukio mengi ya ajali na kusababisha vifo na ulemavu.
Pia wito umetolewa kwa wadau mbalimbali nchini na nje ya nchi ambao watapenda kusaidia jitihada hizo za Athumani Hamisi kuchangia ama moja kwa moja kwake au kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ambayo Mwenyekiti wake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nadani, Pereira Silima na Katibu ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga.

Athumani
ni Mwandishi wa habari wa shirika la Magazeti ya Serikali, Tanzania
Standard Newspapers (TSN), inayochapisha magazeti ya Daily News na
Habari Leo na alipata ajali ya gari huko Rufiji takribani miaka mitano
iliyopita hali iliyompelekea ulemavu ambapo viungo vya mwili wake
vimepooza.
No comments:
Post a Comment