KOCHA
Mkuu wa Coastal Union ya Tanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amepanga kujiunga na
timu ya CDA ya Dodoma ,
aliyowahi kuichezea katika maisha yake ya soka kabla ya kuwa miongoni mwa nyota
mahiri nchini.
Julio
aliyewahi kuichezea Simba na timu ya soka ya Tanzania , Taifa Stars, alitua
Coastal Union ya Tanga mabingwa wa Bara wa mwaka 1988, mwishoni mwa raundi ya
kwanza ya Ligi Kuu, akichukua nafasi ya Hafidhu Badru.
Akiwa
na Coastal Union, aliiwezesha kufanya vizuri katika mechi kadhaa za raundi ya
kwanza na kuchanua zaidi katika raundi ya pili ambapo kwa sasa, inakamata
nafasi sita kwenye msimamo wakiwa na pointi kwa pointi 35 sawa na Mtibwa Sugar,
alikiwa wakiachwa kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Akithibitisha
hilo jana
kupitia kipindi cha michezo cha Radio Uhuru, Julio alisema si kitu cha ajabu
kurejea katika timu yake ya zamani kuisaidia katika jitihada za kutaka kurejea
Ligi Kuu.
“Sio
kitu cha ajabu mimi kuifundisha CDA, timu yangu ya zamani niliyowahi kuichezea
huko nyuma, nikiiacha Coastal Union katika Ligi Kuu, hiki ni kitu cha kujivunia
kwa wadau wote wa Tanga,” alisema Julio.
Alisema,
ingawa kwa sasa bado hajamalizana na viongozi wa timu hiyo, lakini ameamua
kujiunga nayo kwa lengo la kuiwezesha kurejesha hadhi na heshima yake katika medani
ya soka nchini.
Hivi
karibuni, CDA ilitangazwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Taifa Mkoa wa Dodoma , lakini wakawa
wanapingwa na timu ya Maskani, wakijenga hoja kuwa wao ndio walistahili kupewa
heshima hiyo.
No comments:
Post a Comment