Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 17, 2012

WASHINDI WA KILIMANJARO MUSIC AWARD KUFANYA ZIARA MIKOANI


Meneja wa kinywaji cha bia cha Kilimanaro Lager akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Savannah Lounge jijini Dar es salaam kuhusua ziara ya washindi wa tuzo za Kilimanjaro Music Award, Katikati ni mwanamuziki Diamond na kushoto ni Mwakilishi wa EATV Olympia Franteu.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa Kilimanjaro Music Awards leo wamezindua rasmi ziara ya washindi wa tuzo hizi kwa mwaka 2012.

Ziara hizi zitakazofanyika katika mikoa 6 ya Tanzânia zitahusisha uvumbuzi wa vipaji vichanga vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya. Mikoa itakayohusishwa ni Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara na kilele kuwa Dar es Salaam.
Ziara hii ya aina yae itajumuisha wasanii walioshinda tuzo za muziki za Kili, na hão watakaozinduliwa kwenye mikoa husika na kuwapa nafasi wasanii hão chipukizi kushiriki kikamilifu na kuonyesha vipaji vyao kama mpango wa bia ya Kilimanjaro wa kuzindua vipaji.

“Tunataka kuondoa mawazo hasi yaliyopo kwamba Tuzo za muziki za Kili ni za Dar es Salaam tu. Mwaka huu bali na kuwapeleka washindi wa tuzo mikoani tumeamua pia kuzindua vipaji vipya kweye mikoa hiyo kwani tunaamini kuwa vipaji vya muziki vinapatikana Tanzânia nzima. Vilevile tutawapa nafasi wasaniii watakaovumbuliwa kuimba na washindi vinara wa tuzo za Kili ambapo mshindi mmoja wa kila mkoa ataletwa Dar es Salaam kushiriki kwenye tamasha la mwisho la ziara, na pia kurekodiwa nyimbo moja ya kumwezesha kuanza safari yake ya muziki.” Alisema George Kavishe meneja masoko wa bia ya Kilimanjaro.

Kati ya wasanii watakaoshiriki kwenye ziara hizi za washindi wa tuzo za Kili ni pamoja naDiamond, Khadija Kopa, Suma Lee, Warriours from the East, Ali Kiba, AT, Aisha Msharuzi, Twanga Pepeta, Ben Pol, Roma, Ommy Dimples, Kalijo Kitokololo, Jaguar na Barnaba. Msanii mahiri Diamond ambaye amejinyakulia tuzo 3 kwenye tuzo za Kili wiki iliyopita alisema “Nina furaha kubwa kuwa kati ya washiriki wa ziara hizi, ni nafasi ya kipekee kwa mimi kukutana na mashabiki wangu walioko mikoani na kuwaonyesha shukurani zangu kwa upendo wao kwangu” Mbali na ziara hii kutegemea kuongeza mshikamano wa watanzania kwenye kushabikia muziki wa ndani pia itaongeza msisimko wa watanzania kushabikia wasanii wetu mahiri.
Ziara za tamasha zitaaza mkoani Dodoma tarehe 28 Aprili (Jamuhuri Stadium), - Mwanza tarehe 5 Mei (CCM Kirumba), Kilimanjaro tarehe 12 Mei(Ushirika Stadium), Mbeya tarehe 19 Mei (Sokoine Stadium), Mtwara tarehe 26 mei (Mtwara Stadium) na Dar es Salaam tarehe 2 June (leaders club).

Uvumbuzi wa vipaji utafanyika kwenye mikoa mitano kila mwisho wa juma, wiki moja kabla ya tarehe ya tamasha, ikianza na Dodoma tarehe 22 April (Club 84), Mwanza tarehe 29 April(Villa Park), Kilimanjaro tarehe 6 Mei (Mr. Price- Moshi), Mbeya tarehe 13 Mei (Vibes) na Mtwara tarehe 20 Mei (Maisha club).



Majaji wa kuamua mchakato wa uvumbuzi wa vipaji ni pamoja na Juma Nature, Proffessor Jay na Queen Darleen. “ Nikiwa kama mdau wa siku nyingi wa muziki wa kizazi kipya nchini natumaini nitatoa mchango mkubwa kwenye zoezi hili la kuzindua wasanii chipukizi mikoani. Nategemea kuona washiriki wa ike wakijitokeza kwa wingi kwani kuna pengo kubwa sana la uchache wa wasanii wa kike nchini” alisema msanii Professor Jay..

“Tunawaasa wenye vipaji vya musiki kujitokeza kwa wingi na kushiriki kwenye mchakato huu wa kuzindua vipaji ili wapate nafasi ya kuendeleza vipaji vyao” alimalizia bwana Kavishe.

Ziara nzima itarekodiwa na kuonyeswa kwenye kwenye televisheni ya EATV ambapo watanzania watapata nafasi ya kujionea jinsi mchakato mzima wa kuvumbua vipaji na matamasha yalivyoenda.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...