Na MWANDISHI WETU
MWAKILISHI wa Wanawake na Maendeleo ya Vijana, Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena' Mama Kanari Kipingu' ametembelea kambi ya timu ya ngumi ya Taifa na kuwaasa wawe makini wanapokwenda kwenye michuano ya kufuzu mashindano ya Olimpiki.
Akizungumza na mabondia hao kambini kwao Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani jana,' Mama Kanari Kipingu' alisema licha ya kwamba kambi ilikuwa na ugumu wa aina fulani lakini wahakikishe wanarudi na medali kwa watu wote watakaokwenda katika mashindano hayo.
Alisema anajua mabondia wote wapo katika hali nzuri na pia nafasi za kufuzu michuano hiyo ni chache hivyo wanatakiwa kufanya mazoezi kwa bidii kwani siku zilizobaki ni chache.
"Nimeamua kuja kuwatembelea ili kuwapa hamasa na mjue kama tupo nyuma yenu, lakini sitaondoka bure ninawapa hii sh. 50,000 kwa ajili ya kununulia maji na vitu vingine vidogo vidogo na kwamba bondia atakayerudia na medali ataandaliwa zawadi maalum na BFT," alisema' Mama Kanari Kipingu'
Alisema kesho jumatatu watakuwa na kikao ambacho kitajadili ni zawadi gani watakayotoa kwa bondia atakayerudi na medali na pia aliahidi kuisaidia BFT kulipa deni wanalodaiwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (AIBA).
Katika hatua nyingine, Zuwena ambaye anaupenda sana mchezo huo, alisema yupo mbioni kutoa tuzo kwa makocha ambao walifanya vizuri katika miaka iliyopita lakini bado mpaka hivi sasa wanauendeleza mchezo huo
No comments:
Post a Comment