Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 4, 2013

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAASWA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA WANAZOZALISHA


DSC_0394
Mama Tunu Pinda akikaribishwa kufunga maonyesho ya wiki ya Wakinamama Wajasiriamali na Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza wajasirimali wanawake Tanzania kutoka ILO, Noreen Toroka. kushoto kwa Mama Pinda ni Mwenyekiti wa MOWE, Bi Elihaika Mrema na
DSC_0354
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akifunga rasmi Maonyesho ya Wanawake Wajasirimali (MOWE) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, maonyesho hayo ya wanawake wajasiriamali yalikuwa ya wiki nzima ambapo wakinamama wanapata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa mbalimbali Usindikaji, Mvinyo, Batiki kwa wakazi wa jijini.
DSC_0337
Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali kwa wanawake Tanzania toka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka akizungumza wakati hafla ya kufunga maonyesho hayo ambapo amesema wiki nzima ilikuwa ni maonyesho wanawake toka sehemu mbalimbali nchini Bara na Visiwani wamepata wasaa wakubadilishana mawazo na mbinu za Kibiashara.
DSC_0324
Mwenyekiti wa Kamati ya MOWE, Mama Elihaika Mrema akizungumza wakati wa kufunga maonyesho hayo ya Wajasirimali wakinamama jijini Dar es Salaam.
DSC_0287
Mama Tunu Pinda akitembelea baadhi ya mabanda katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
DSC_0302
Mama Tunu Pinda akipata maelezo kwa mmoja wa Wajasirimali Wanawake walioshiriki maonyeshio hayo.
DSC_0381
Mgeni rasmi Mama Pinda akikabidhi vyeti kwa mmoja wa washiriki wa maonyesho (Certificate of Participation).
DSC_0367
Mgeni rasmi Mama Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji Wake na viongozi wa MOWE.
DSC_0356
Mama Tunu Pinda akiserebuka na baadhi ya Wanawake Wajasiriamali wakati wa sherehe za kufunga maonyesho hayo. .Watanzania wahimizwa kununua bidhaa zinazotengenezwa na wazawa
Na Damas Makangale, MOblog

WANAWAKE Wajasiriamali nchini wameaswa kuzingatia umuhimu wa ubora kwenye bidhaa zao wanazozalisha kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa ili kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi. Moblog linaripoti.

Akizungumza kwenye kilele cha wiki ya Wajasiriamali Wanawake Tanzania (MOWE) Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wanaweza kufanikiwa endapo watazingatia ubora wa vifungashio (Packaging) wanavyotumia kwenye bidhaa zao.

“Nimedokezwa kwamba baadhi ya wajasirimali wamejisajili na kupata kiandishi-anuani yaani Barcodes, hapa Tanzania, mfumo huu umeanza kutumika hivi karibuni na wajasirimali wengi wameshawishiowa kujiunga ili bidhaa zao ziweze kutambuliwa kitaifa na kimataifa,’ amesema
Mama Pinda amesema kwamba watanzania wote wake kwa waume lazima wapende kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nyumbani ili kuweza kuwainua wajasirimali wazawa hasa wakinamama kwa kuunga mkono kampeni ya “Be Tanzanian, Buy Tanzanian” inayohimiza kuwa Mzalendo, Nunua bidhaa za kitanzania.

Amesema hata hivyo, kuna baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na baadhi ya vikundi vya hapa nyumbani bado hazijaweza kumudu ushindani wa soko na kukubalika kuuzwa kwenye maduka makubwa yaani supermarkets.

Mama Pinda aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa inayowakabili wajasirimali wenhi ni kutozingatia viwango vinavyotambulika katika soko la ndani la nje ili bidhaa za wazawa ziweze kupenya kwenye soko la kitaifa, kikanda na kimataifa kwa maslahi mapana ya wajasirimali na nchi kwa ujumla.

“kwenu akinamama wajasiriamali na wale waliohidhuria wasio wajasiriamali ni matumaini yangu kuwa mmetumia fursa hii kubadilishana mawazo na kujenga mitandao ya kusaidiana na kuendelezana,” alisisitiza

Kwa upande wake, Mratibu wa kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali kwa Wanawake Tanzania kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka amesema shirika la kazi linafarijika kuchangia katika mipango na program za serikali za kuchangia ukuaji wa ajira kwa kupitia program za ILO katika kumuendeleza mjasiriamali mwanamke nchini.

“kwa takribani miongo miwili ILO imekua ikifanya kazi kuhakikisha ujasirimali unachangia ajira na kipato kwa kina mama na tunajivunia kuwa kati ya wadau wengi walio katika kujengea uwezo washirika wetu idara za serikali, asasi za kifedha na zisizo za kifedha katika kuwainua wajasiriamali wakinamama Tanzania,” amesema 

Toroka amesema katika kuendeleza wakinamama nchini ILO imetoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake zaidi ya 500 na kuwaunganisha na huduma za kifedha na wataalamu wa ujasiriamali kwa elimu ya biashara na stadi za kazi.

“Kupitia washirika wetu ILO imefikia wakina mama 100 Mkoani Lindi na tunashukuru wadau wtu WAMA Foundation na program yao ya village savings and loan, wakinamama hao walipata mafunzo ya ujasiriamali na tunategemea watapata mikopo nafuu ili waweze kuanzisha, kuboresha na kupanua biashara zao,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...