Mkurugenzi wa Huduma kwa
Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa
kitengo cha huduma kwa wateja na
maongezi na Bwana Aliasger Hussein wakati Airtel ilipomtembelea ofisini
kwake katika wiki ya huduma kwa wateja. Pichani ni Meneja huduma kwa wateja
Jacob Sumary na Afisa huduma kwa wateja bi Neifita Olomi
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imehitimisha wiki hii inayosherehekewa duniani kwa kuwatembelea wateja
wake mbali mbali na kuwashukuru kwa kutumia huduma na bidhaa zake.
Airtel imetembelea wateja wake katika maeneo mbalimbali ikiwa pamoja na
Tandika, magomeni, Temeke ,Sinza, Mbagala, illala , kinondoni na katika maeneo
yenye watu wengi na kuongea nao kwa nyakati tofauti lengo likiwa ni kupata
maoni juu ya huduma na pia kuwaelimisha kuhusu huduma na ofa mbalimbali.
Alikadhalika wakurugenzi wa Airtel walitembelea
wateja katika ofisi zao na kutembelea call center kituo cha kuhudumia wateja
waaopiga simu na kuongea na wateja wanaopiga namba 100 kwa msaada zaidi.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha wiki hii Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa
wateja Bi Adriana Lyiamba alisema” tumekuwa na wiki ya mafanikio makubwa kwani
tumepata nafasi nzuri ya kuendelea kuonana na kuongea na wateja wetu ana kwa
ana na kuwazawadia ikiwa ni kuwashukuru kwa kuwa pamoja nasi na kutumia huduma
zetu.
Tunaahaidi kuendelea
kutoa huduma bora zilizo za kisasa na za kibunifu huku tukitoa huduma kwa
wateja zenye uzoefu tofauti kupitia kituo chetu cha kupokea simu (call center)
maduka yetu na sehemu zote ambazo wateja wanapata huduma zetu. Tunapomaliza
wiki hii maalumu kwa huduma kwa wateja tunapenda kuwahakikishia watanzania
huduma bora kwani tunatambua huduma bora ni mwendelezo wa maisha ya kila siku
na si kwa wiki hii tu.
Akiongea wakati alipotembelewa ofisini kwake Bwana Aliasger Hussein Gomberawala
alisema” tunafurahi kwa uongozi wa Airtel kuwa nasi leo hapa, tumekuwa wateja
wa Airtel kwa muda na tunafurahishwa na huduma zao kwa ujumla, matatizo ya
kimtandao katika technologia hii yapo mengine ni ya uelewa wa vifaa vya kisasa
na technologia hivyo elimu inatakiwa kutolewa ili wateja waende sambamba na
mabadiliko haya.
Tunaomba Airtel waendelee kutuletea huduma za kibunifu na kuendelea kupunguza
gharama za mawasiliano kwani tunategemea sana haya mawasiliano katika kuendesha
biashara zetu.
No comments:
Post a Comment