Bondia Ally Bugingo akipima uzito kwa
ajili ya mpambano wake na Amani Bariki 'Manny Chuga' mpambano
utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends corner Manzese Dar es
salaam katikati ni Antony Rutta picha na SUPER D BLOG
Bondia Sadiki Nuru akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho jumamosi
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kwa
ajili ya mpambano wake utakaofanyika kesho oktoba 25 katika ukumbi wa
frends corner manzese ambapo anapambana na George Dimoso mpambano wa
raundi nane picha na SUPER D BLOG
Bondia Fadhili Boika kushoto
akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya kupima uzito kwa ajili
ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba 25 katika ukumbi wa
Frends Corne Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG
Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika
October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka
kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya
mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Trust Rating
Not Yet Rated
No comments:
Post a Comment